24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mama mjamzito afariki kwa kutumbukia mtoni

Na GURIAN ADOLF-KALAMBO

MWANAMKE mjamzito, aliyefahamika kwa jina la Maria Kalunde (42), pamoja na mtoto wake Magreth Lui (9) wamekufa maji baada ya kutumbukia katika Mto Kalambo kutokana na kuteleza katika kivuko cha miguu cha mto huo.

Tukio hilo limetokea jana katika Kijiji cha Kasitu Kata ya Sopa wilayani Kalambo mkoani Rukwa wakati watu hao wakivuka katika mto huo.

Akizungumzia tukio hilo mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Nobert Mwanawima alisema mwanamke huyo mjamzito pamoja na mtoto wake walikufa maji kutokana na eneo hilo kutokuwa na daraja la kuvukia kitendo kilichosababisha wananchi wa kijiji hicho kutengeneza kivuko cha miguu kinachokatisha mto kwa kutumia miti.

Alisema kuwa mwanamke huyo alipokuwa akipita katika kivuko hicho pamoja na mwanaye waliteleza na kuangukia mtoni, na kisha walianza kupiga kelele za kuomba msaada, lakini kwakuwa watu walikuwa mbali hawakufanikiwa kufika kwa wakati kuwasaidia.

“Siku mbili baadaye walipata taarifa kuwa miili yao ilipatikana katika kijiji jirani na wakazi wa kijiji hicho baada ya kuona kuwa watu hao hawafahamiki waliamua kufanya maziko, ndipo walipoamua kuchukua  msiba na kuusafirisha hadi kijiji cha  Katete walipokuwa wakiishi mama huyo pamoja na mwanaye,” alisema 

Naye Jeremia Shigoma mkazi  wa Kijiji cha Kasitu, alisema kuwa kutokana na changamoto ya kutokuwa na daraja katika  eneo hilo watu wamekuwa  wakifa maji kutokana na kusombwa na maji hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika nyakati za masika kwakuwa mto huo unakuwa umejaa maji.

Aliiomba serikali kuwajengea daraja katika eneo hilo ili kuepukana na vifo vinavyotokea mara kwa mara kwani wao wamekuwa hawajisikii vizuri kushuhudia watu wakipoteza maisha kila nyakati za masika.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Gasper kateka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa,  awali hali ilikuwa mbaya zaidi kwakua hakukua hata hicho kivuko lakini kilipatikana baada yawananchi  kujichangisha  fedha  kiasi  cha Sh 10,000 kila mmoja kwaajili ya kuwalipa mafundi waliokitengeneza.

Diwani wa kata hiyo,  Richad Kamagari (CCM), alisema tatizo la vifo kutokana na kutumbukia watu mtoni limekuwa likijitokeza mara nyingi na yeye amekwisha toa taarifa katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kalambo.

Kwaupande wake Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kalambo, Mahmood  Shauri , amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  ambapo alisema kuwa serikali itajitahidi kutatua changamoto hiyo inayowakumba wakazi wa kijiji hicho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles