Hong Kong, CHINA
VURUGU zimeshuhudiwa mjini Hong Kong usiku wa kuamkia jana kufuatia makabiliano kati ya polisi wa kupambana na fujo na wanaharakati wanaopigania uhuru na demokrasia zaidi.
Maelfu ya waandamanaji waliovalia mavazi meusi na wengine kofia za Santa (Krismasi), walijitokeza katika barabara za mtaa unaowavutia watalii wengi wa Tsim Sha Tsui.
Maofisa wa polisi wamefyatua risasi za mipira pamoja na gesi za kutoa machozi kwa waandamanaji waliorusha mabomu ya petroli katika sehemu ya maduka mengi.
Makabiliano hayo yalidumu kwa muda mrefu baada ya wiki chache za kurejea kwa utulivu kwenye mji huo ambao umetikiswa na maandamano na vurugu kwa zaidi ya miezi sita sasa.