23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Watoto 212 wazaliwa mkesha wa Krismasi Dar

Na  AVELINE  KITOMARY-DAR ES SALAAM 

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Yudas Ndugile,  amesema katika mkesha wa Krismasi watoto 212 wamezaliwa katika mkoa huo.

Gazeti la MTANZANIA pia lilipita katika hospitali mbalimbali mkoani ili kupata taarifa za uzazi  zaidi ambapo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili watoto waliozaliwa katika mkesha wa Krismasi walikuwa sita, wanne kutoka Upanga na wawili Mloganzia .

Ofisa habari wa Muhimbili, John Stephen, alisema  watoto waliozaliwa wote ni wakike na wamezaliwa kwa njia ya kawaida huku afya za watoto na wazazi zikiendelea vizuri.  

Naye Ofisa Muuguzi wa Hospitali ya Temeke, Hamisa Sadick alisema katika hospitali hiyo watoto waliozaliwa ni 14, watoto pamoja  na wazazi hali zao zinaendelea vizuri.

“Kati ya hao watoto tisa walizaliwa kawaida wa kiume ni wanne na wakike ni watano  na waliozaliwa kwa upasuaji wako watano ambapo wawili ni wakike na watatu niwakiume wote zalizao ni njema,”alisema Hamisa.

Kwa upnade wa Hospitali ya Mwananyamala katika mkesha wa krismasi jumla ya watoto 19 walizaliwa  kati ya hao 14 ni wakike na watano  ni wakiume.

“Watoto waliozaliwa kwa njia ya kawaida wakike ni 12 na wakiume ni wane  na waliozaliwa kwa upasuaji wawili walikuwa wakike na mmoja wakiume lakini wote hali zao zinaendelea vizuri,” alisema Muuguzi Abdul Mohamed.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles