26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Makonda kuwaongoza Watanzania mapokezi timu ya taifa Olimpiki

Paul Makonda
Paul Makonda

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, atawaongoza Watanzania na wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika mapokezi ya timu ya taifa ya kuogelea inayotarajia kuwasili kesho kutoka jijini Rio de Jeneiro, Brazil katika michezo ya Olimpiki.

Timu hiyo inayoundwa na waogeleaji, Magdalena Moshi na Hilal Hilal, wakiwa chini ya kocha wao Mkuu, Alexander Mwaipasi, inatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 9 alasiri.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhani Namkoveka, aliliambia MTANZANIA jana kuwa timu hiyo imeanza safari jana kutoka jijini Rio kuelekea Sao Paulo kabla ya kuelekea Dubai leo.

“Timu itaondoka Dubai UAE siku ya Alhamis asubuhi (kesho) na kuja moja kwa moja Dar es Salaam kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates,” alisema.

Namkoveka aliwataka Watanzania na wakazi wa jiji kujitokeza kwa wingi kuipokea timu hiyo ili kuipa moyo kwani licha ya kukosa medali lakini imeiwakilisha vema Tanzania.

“Watanzania waje ili yawe mapokezi makubwa, hii ni kutokana na ukweli kuwa wachezaji wetu wameliwakilisha vema taifa hasa pale Hilal alipoipeperusha bendera ya Tanzania na kuweka rekodi mpya ya taifa ya sekunde 23.70,”

“Katika mtindo wa ‘freestyle’ mita 50, rekodi ambayo haijawekwa na Mtanzania yeyote, pia TSA inawashukuru wale wote ambao wamekuwa pamoja nasi na tunawaahidi kuwa kazi ya kuueneza mchezo huu ndo inaanza sasa,” alisisitiza katibu huyo.

Waogeleaji Magdalena na Hilal wanarejea nchini bila medali baada ya kushindwa kufurukuta katika michezo hiyo inayoendelea jijini Rio de jeneiro Brazil.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles