27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wafuasi wa upinzani wakamatwa Zambia

image-20160805-484-37093z

LUSAKA,

POLISI nchini hapa wamewakamata watu 133 wanaopinga ushindi wa Rais Edgar Lungu, baada ya mshindani wake mkuu Hakainde Hichilema, kudai kuwa kura ziliibwa katika uchaguzi wa urais.

Maandamano yalizuka katika sehemu nyingi za Mkoa wa Kusini ukiwemo mji maaarufu kwa utalii wa Livingstone.

Mkuu wa Polisi Godwin Phiri, aliliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa waandamanaji walikuwa wakiwalenga wafuasi wa chama tawala na kisha kuharibu mali zao.

“Ni mpango uliopangwa vyema na walikuwa wakisubiri mshindi atangazwe. Utulivu sasa umerejea kutokana na kufanyika kamata kamata,” aliongeza.

Hichilema anasema kuwa ana mpango wa kupeleka kesi mahakamani kupinga matokeo hayo.

Licha ya malalamiko ya upinzani kuhusu wizi na udanganyifu wa kura, Lungu alitangazwa na Tume ya Uchaguzi kutetea urais kwa kupata asilimia 50.35 katika uchaguzi wenye ushindani mkali ambao ulifanyika Alhamisi iliyopita.

Mpinzani wake mfanyabiashara Hichilema kutoka Chama cha United Party for National Development (UPND) alipata asilimia 47.67 ya kura.

Upinzani nchini umeishutumu Tume ya Uchaguzi (ECZ) kuingia makubaliano ya kumpendelea Rais Lungu na ameapa kupinga matokeo hayo katika Mahakama ya Katiba.

Rais wa chama cha Movement for Multiparty Democracy MMD), Dk Nevers Mumba, amesema analo mkononi pingamizi la kuzuia matokeo yasitangazwe, jambo ambalo lilipuuzwa na tume.

“Tulienda mahakamani Jumapili na tukapewa pingamizi la kuzuia ECZ isiendelee kutangaza matokeo ya uchaguzi na wakapuuza agizo la mahakama na kuendelea kutangaza kura zenye mgogoro,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles