27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

MAKOCHA WATISHIA KUGOMEA RBA

Na SHARIFA MMASI-DAR ES SALAAM

MAKOCHA mbalimbali ambao timu zao zinashiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), wametangaza kugoma kucheza hatua ya robo fainali hadi hapo uongozi wa Chama cha Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), utakapotekeleza mahitaji yao.

Moja ya mahitaji wanayodai ni kurudishwa katika nafasi yake mmoja wa kiongozi aliyekuwa Kamishna Ufundi na Mipango wa BD, Halleluya Kavalambi, aliyevuliwa cheo kwa madai ya kukiuka kanuni na taratibu za chama hicho.

Kwa mujibu wa nakala iliyoonekana kusambaa mitandaoni iliyosainiwa na makocha 10 wanaopinga kuondolewa kwa Kavalambi, makocha hao wanatishia kususia robo fainali ya ligi hiyo inayoendelea hadi kiongozi huyo atakaporudishwa.

Mmoja wa viongozi ambaye timu yake inashiriki RBA msimu huu (jina linahifadhiwa), alisema wanahitaji kukaa na uongozi wa BD uliopo madarakani kwa lengo la kutatua dosari na changamoto zinazoendelea kutafuna mafanikio na maendeleo ya kikapu nchini.

Msemaji wa BD, Peter Mpangala, akizungumzia juu ya suala hilo alisema kuwa yupo kwenye kikao na taarifa rasmi itatolewa baadaye.

Hata hivyo, baadaye alipotafutwa alisema kuna baadhi ya makocha wanatishia kugoma, lakini mzunguko wa pili utaendelea Jumatano kama kawaida.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles