26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

JAY-Z: AMY WINEHOUSE HAKUTUSIKILIZA

NEW YORK, MAREKANI

RAPA Jay-Z, amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa muziki nchini Uingereza, Amy Winehouse, akidai kuwa msanii huyo hakusikia ushauri wake.

Amy alikutwa amepoteza maisha nyumbani kwake jijini London, Julai 23, 2011, kifo hicho kilitokana na matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya.

Jay Z amedai kwamba, mara ya kwanza kukutana na msanii huyo jijini New York alimtaka kuungana pamoja, lakini Amy alionekana wazi kuwa hataki.

“Mara ya kwanza kukutana naye niliamini kuwa ana uwezo mkubwa wa kuimba, nilimwomba aungane na sisi lakini hakuonesha kukubali, nilikuwa na lengo la kutaka kumbadilisha ili aweze kuachana na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na pombe, lakini hakutusikiliza,” alisema Jay Z.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles