25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

MAKATIBU 20 WA MIKOA CCM WANG’OLEWA

Na ESTHER MBUSSI-DAR ES SALAAM


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimefanya mabadiliko ya   makatibu wa mikoa 30 na wilaya 155 wa chama hicho nchini.

Kati yao, makatibu wapya wa mikoa ni 20 na wa wilaya 70,  huku asilimia 30 ya viongozi hao wakiwa wanawake.

Katika mabadiliko hayo, wamo makatibu wa wilaya wa zamani waliopandishwa  kuwa makatibu wa mikoa wakati wengine wamehamishwa mikoa akiwamo wa Mkoa wa Shinyanga  ambaye amehamishwa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaam jana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole,  alisema uteuzi huo ni mwendelezo wa mageuzi ambayo yanaendelea kufanyika ndani ya chama hicho.

Alisema uteuzi huo umelenga kuhakikisha unakuwapo ufanisi katika maeneo matatu ambayo ni mageuzi ya uongozi,  mfumo wa  utawala na utendaji.

“Tunataka kuhakikisha mageuzi hayo yanaongeza tija na ufanisi katika kuwa na viongozi wawajibikaji katika mtawanyo wa wanawake na wanaume na ambao wanakidhi vigezo vya uongozi na kuachiana vijiti katika utendaji.

“Tunataka kuwa na aina ya viongozi ambao ni waadilifu na wenye weledi na uzoefu ambao unajitosheleza.

“Tumekuwa madhubuti kwa wale wanaotafuta vyeo nje ya mfumo wa kanuni za chama.

“Tunataka viongozi katika chama chetu ambao watapatikana bila rushwa na kutoruhusu mianya ya kuwaruhusu watu kuleta mamluki ndani ya chama,” alisema.

Apoulizwa kuhusu taarifa kuwa  Katiba ya chama hiyo imebadilishwa kuruhusu mgombea urais kupita bila kupingwa baada ya kipindi cha miaka mitano, Polepole alisema si kweli.

Alisema  mgombea wa nafasi hiyo kupitia chama hicho atawekwa wazi mwaka 2020.

“Tunaheshimu watu kutoa mawazo yao kupitia katiba yetu lakini kuna wachache wanaopotosha kwa makusudi… tunawaomba kupuuzia taarifa hizi,” alisema Polepole.

Baadhi ya makatibu na mikoa wanayokwenda katika mabano ni aliyekuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Elias Mpanda (Arusha),  Katibu wa  Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe (Dar es Salaam), Katibu Msaidizi, Jamila Yusuf (Dodoma),  Katibu wa  Mkoa wa Mara, Adam Ngalawa (Geita) na Mkuu wa Wilaya ya Newala wa zamani, Christopher Magala (Iringa).

Wengine ni Katibu wa CCM Kagera, Rahel Degeleke (Kagera), Katibu wa  Wilaya ya Babati Mjini, Kajolo Peter (Katavi), Katibu wa   Kigoma, Naomi Kapambala (Kigoma), Katibu wa Wilaya ya Kinondoni, Jonathan Marko (Kilimanjaro),  Katibu Wilaya ya Masasi, Mwanamasoud Pazi (Lindi) na Mkuuwa Wilaya ya Mpanda wa zamani, Paza Mwamlima (Manyara).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles