24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Makalla awataka wananchi kuchukua tahadhari ya corona

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kufuatia kuwepo kwa viashiria vya Mlipuko wa Ugonjwa wa corona, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukua tahadhari na kuziagiza Taasisi na sehemu zote za mikusanyiko kuweka ndoo za maji na miundombinu ya maji tiririka.

Akitoa tamko la tahadhari dhidi ya corona leo Alhamisi Juni 24, 2021 Makalla amesema kutokana na Mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani na nchi mbalimbali na Mikoa mingine wameona ni vyema kutoa tahadhari kwa wananchi.

Miongoni mwa tahadhari ambazo Makalla amewataka wananchi kuzichukuwa ni pamoja na;

“Kuvaa kwa Usahihi Barakoa kila wawapo sehemu za mikusanyiko, vyombo vya usafiri, Masoko, sherehe, maofisini na vituo vya Afya, kunawa mikono kwa maji tiririka kwa sabuni mara kwa mara. Wananchi kuwahi mapema vituo vya Afya wanapobaini dalili za Corona ikiwemo homa Kali, mafua Makali, kikohozi, uchovu na nyingine.

“Kufanya mazoezi ili kuimarisha kinga ya mwili, kula mlo kamili, uangalizi mzuri kwa watu walio kwenye hatari ya kupata madhara wakiwemo Wazee na wenye magonjwa sugu,” amesema Makala.

Aidha, Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma na za kiraia na Vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia ipasavyo maelekezo hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles