Oman: Israel acheni Palestina ijitawale

0
766

Muskat, Oman

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr al-Busaidi, anaamini Serikali mpya ya Israel itaifanya Palestina kuwa nchi huru.

Al-Busaidi amesema hayo akizungumza kwa simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Yair Lapid, kwa mujibu wa Shirika la Habari la ONA la Oman.

Alichokisema Al-Busaidi ni kwamba Palestina inapaswa kuachwa isimame, ikiwamo kuikabidhi East Jerusalem kuwa makao makuu yake.

Katika hatua nyingine, al-Busaidi amesema Oman inaridhidhwa na uhusiano wkae na Israel, ikiwamo Serikali mpya chini ya Waziri Mkuu, Naftali Bennett.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here