22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Bila chanjo, hupati kazi kwenye ndege

Shenzhen, Hong Kong

Shirika la Ndege la Cathay Pacific la Hong Kong limetoa sharti la kila mfanyakazi wake kupata chanjo ya Corona, likienda mbali zaidi kwa kusema ‘asiyetaka. basi aache kazi’.

Kwa mujibu wa agizo la uongozi wa Shirika hilo, kila mfanyakazi, hasa wale wanaosafiri na abiria, anatakiwa awe ameshachanjwa ifikapo Agosti 31, mwaka huu.

Aidha, taasisi hiyo ikasema tayari asilimia 90 ya marubani wake wameshapatiwa chanjo, kama ilivyo asilimia 65 ya wahudumu.

“Baada ya umakini wa kutosha, tumeamua kwamba wahudumu wote wa ndege walioko Hong Kong wanatakiwa wawe wameshapata chanjo kufikia Agosti 31, mwaka huu,” inaeleza taarifa ya Shirika hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,167FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles