29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

MAJERUHI AJALI YA WANAFUNZI WAFANYIWA UPASUAJI MAREKANI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

MAJERUHI watatu wa ajali iliyoua walimu wawili, wanafunzi 32 na dereva wa Shule ya Msingi Lucky Vincent jijini Arusha waliopelekwa nchini Marekani, wamefanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Mercy Medical.

Ajali hiyo ilitokea Mei 6 mwaka huu wakati wanafunzi hao na walimu walipokuwa wakienda wilayani Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema na wanafunzi wenzao wa Shule ya Tumaini Junior School.

Majeruhi hao watatu ambao ni Doreen Mshana, Sadia Awadhi na Wilson Tarimo walipelekwa nchini Marekani, Jumapili iliyopita kwa matibabu zaidi.

Katika ukurasa wake wa Facebook jana, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ambaye aliwatafuta wafadhili, alisema mtoto Doreen ambaye alionekana kuumia zaidi alifanyiwa upasuaji kwa saa tisa.

Alisema Doreen alifanyiwa upasuaji kwenye ‘hip’ na mabega jana na madaktari bingwa watatu kwa takribani saa nne kwa mafanikio.

Alisema pia Doreen alifanyiwa upasuaji kwenye taya na Dk. Bingwa Jeff Dean kwa muda wa saa tano.

“Mtoto Doreen alifanyiwa upasuaji kwenye 'hip', na 'shoulder' jana na madaktari bingwa watatu kwa takribani saa nne kwa mafanikio makubwa, pia alifanyiwa upasuaji kwenye 'Jaw' (taya) na Dk. bingwa Jeff Dean kwa muda wa saa 5 juzi.

 “Siku ya kesho (leo) Alhamisi, Doreen atafanyiwa upasuaji wa 'spine' na madaktari bingwa watatu walioandaliwa kwa shughuli hiyo muhimu.

“Maktari wanasema, kuanzia saa tano usiku kwa saa za CST-Sioux City IA, Doreen kwa mara ya kwanza tangu aingizwe OR, ameanza kujisikia hisia (feelings) kwenye mguu wake wa kulia. Sote tuendelee kutuma dua, sala na upendo wetu kwake,”alisema Nyalandu.

Aidha alisema mtoto Sadia na Wilson wote walifanyiwa upasuaji huku kila mmoja akiwekwa kwenye chumba cha peke yake wakiangaliwa na mama zao pamoja na nesi.
 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles