30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

WALIOMUA OCD UVINZA WAKAMATWA

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

SIKU moja baada ya kuuawa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma,  Amedeus Malenge, watu wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo wametiwa mbaroni.

Watuhumiwa hao walikamatwa usiku wa kuamkia jana, Kinyezi Kanga   Dar es Salaam, baada ya msako mkali uliohusiha askari wa kikosi maalumu kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi kiliambia MTANZANIA jana kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuhusishwa na tukio hilo la mauji ya kinyama.

Malenge ambaye ambaye alihamishiwa wilayani Uvinza akitokea Kibaha mkoani Pwani ambako alikuwa Ofisa Upelelezi wa wilaya, aliuawa   juzi   saa 4.00 usiku.

 “Ni kweli wamekamatwa baada ya msako mkali wa polisi,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakutaja kutajwa jina gazetini kwa kuwa si msemaji wa polisi  na kuongeza:

“Marehemu alikuwa anapita na gari yake jirani ya nyumba yake moja ambayo bado haijaisha. Akiwa katika hilo eneo alimuona mtu mmoja ambaye walikuwa wakifahamiana akilalamika kuwa kuna watu walikuwa wanataka kumuua huku akimwita kwa jina ili amsaidie.

“Marehemu aliposhuka   aliuliza ‘kulikoni mbona mnataka  kumpiga, kulikoni’.

“Ghafla alitokea mtu kwa nyuma akampiga kwa shoka kichwani   akafariki papo hapo”.

  MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilipolisi wa Ilala, Salum Hamduni   kupata ufafanuzi wa suala hilo, simu yake ilipokewa na msaidizi wake ambaye alisema alikuwa  kwenye majukumu ya kazi.

“Mimi si kamanda ila mimi ni msaidizi wake, kamanda yupo kwenye majukumu na kama unamhitaji atakupigia baada ya muda wa dakika 10 kutoka sasa,” alisema msaidizi huyo wa Kamanda Hamduni na kukata simu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles