25.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 30, 2022

Contact us: [email protected]

Majambazi yavamia yaua na kupora fedha

Ahmed Msangi
Ahmed Msangi

Na MASYENENE DAMIAN-MWANZA

MTU mmoja amefariki dunia kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi baada ya kuvamia na kupora kiasi cha fedha ambacho hakijafahamika na simu nne za aina mbalimbali katika duka la kuuza vifaa vya ujenzi mtaa wa Nyakato Mecco Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Tukio hilo lilitokea jana saa 1:45 usiku ambapo wavamizi hao ambao idadi yao haijajulikana wakiwa na silaha aina ya SMG walivamia duka la vifaa vya ujenzi mali ya Elikana Ngagaya na kujaribu kupora maduka mengine ikiwa ni pamoja na M-Pesa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alimtaja aliyeuawa kuwa ni Grace Maega (36) Mkazi wa Kangae ambaye alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Inadaiwa wakati majambazi hao wanaondoka eneo la tukio walifyatua risasi tatu zilizompata kwenye bega la mkono wa kushoto wakati akizima taa ndani ya duka lake lililopo jirani na duka tajwa hapo juu kisha wakatokomea gizani.

“Majeruhi alikimbizwaHospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu lakini alifariki dunia masaa machache baadae kwa kuvuja damu nyingi,” alisema.

Katika tukio hilo la unyang’anyi wa kutumia silaha hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na mauaji hayo huku Jeshi la Polisi likiendelea na msako pamoja na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi zaidi. “Tutafanya kila tuwezalo kutumia ujuzi tulionao tukishirikiana na wananchi kuhakikisha tunawakamata majambazi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,436FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles