25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Maisha ya Mo yalivyobadilika baada ya kutekwa

ANDREW MSECHU

MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohamed Dewji (Mo) amesema tangu alipotekwa na watu wasiojulikana Oktoba mwaka jana, maisha yake yamebadilika kutokana na tukio hilo.

Akizungumz akatika mahoijianoi maalumu na Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Mo alisema tangu alipoachiwa Oktoba 20 mwaka jana, baada ya kushikiliwa kwa siku 10 na watekaji hao, kwa sasa mambo si kama ilivyokuwa awali.

“Sasa hivi bado ninaenda mazoezini, lakini natembea na walinzi wengi, maisha yangu ya awali nilikuwa nazururazurura mweyewe, nililkuwa nafanya jogging (mazoezi ya kukimbia) pale Oysterbay mwenyewe, kwahiyo maisha kidogo yamebadilika,” alisema.

Alisem pamoja na kubadilika kwa mtindo wa maisha, bado anaamini kuwa Tanzania ina watu wazuri na watekaji kama waliomteka, wanatoka nje ya nchi na kuja kujaribu kuvuruga amani ya nchi.

 Alisema ametembea mikoa mingi nchini na anawajua vyema Watanzania kuwa ni watu wazuri sana.

Mo ambaye alielezea tukio zima lilivyotokea na maisha yake akiwa mikononi mwa watekaji, alisema kuna watu wengi wanasema kupitia mitandao ya kijamii kuwa amekuwa kimya anaposikia matukio ya utekaji, lakini hawajui ukweli wa kile kilichoko moyoni mwake.

“Hivi ni nani anayejua maumivu ya kutekwa kuliko yule aliyetekwa, mimi likitokea tukio lolote la utekaji, ninaapa kwa Mungu na ninasali kumwomba Mungu asaidie uokozi wa aliyetekwa. Mimi mwenyewe mara nyingi sisemi lakini ndani ya moyo wangu ninamwombea huyu mtu,” alisema.

Alisema kuna maswali mengi lakini mwisho wa yote yeye mwenyewe ni balozi wa kuitetea na kuisemea nchi yake vyema na asingependa kutekwa kwake kusababishe dola lolote kwa nchi.

Maisha kwenye jumba la watekaji

Mo alisema baada ya kutekwa Oktoba 11 mwaka jana, alihifadhiwa kwenye jumba ambalo alibaini kuwa liko ndanindani na kwamba watekaji wake walimfunga mikono na miguu na kumfunga kitambaa machoni wakati wote, tangu walipomteka hadi walipomwachia Oktoba 20 mwaka jana.

Alisema wakati wote, watekaji hao waliwaweka walinzi wawili ambao muda wote walikuwa wanakaa naye na usiku walikuwa wanalala, kwa kuwa alikuwa akiwasikia wakifunga mlango na baadaye wote wawili wakitokomea, huku wakiongea kwa lugha yao.

“Kazi niliyokuwa ninafanya kwanza ni kumuomba Mungu kuwa nitoke salama. Kwenye dini ya Kiislamu kuna sala maalumu. Kwa hiyo nilikuwa nafikiria mabaya niliyowahi kuyafanya na kumwomba Mungu anisamehe kwa kuwa nilishaanza kuona kuna uwezekano mkubwa wa kutotoka salama pale, na mwisho wangu wa maisha unakaribia.

“Nilikuwa nikijitahidi kutofikiria familia kwa sababu kila nilipokuwa nikifikiria watoto wangu ninaanza kulia, kwa hiyo niliona hii kitu itaniweka pabaya na kunivuruga kisaikolojia, kwa hiyo nilianza kublock (kuzuia) kufikiria familia.

“Nilikuwa nafikiria Watanzania, nilikuwa nafikiria watu wangu wa Singida na nilikuwa namwomba tu Mungu.

“Kwa kweli nilikuwa sijui nini kinachoendeela nje, nilijua kuwa lazima watu watakuwa wananitafuta na wao (watekaji) walikuwa wakiniambia kuwa hapa hawawezi kunipata,” alisema.

Alisema kwa muda wote huo hakuwa na nguo bali walimpa kitambaa kama shuka kwa ajili ya kujisitiri na siku aliyotoka ndiyo walimpa shuka aliyokuwa akijifunika

Akizungumzia iwapo utekaji huo unatokana na washindani wake wa kibiashara, Mo alisema kwenye nchi yetu hatujawahi kufika hapo.

“Kuna ushindani wa kibiashara lakini hatujafika mahala huko kwa kuanza kumfanyia mtu mabaya kama haya, na Watanzania kwa ujumla ni watu wastaarabu na watu wazuri.

“Fikra ya kwanza ni kwamba hao watu walikuwa wanataka pesa na siku ya kwanza asubuhi yule jamaa alipigiwa simu nikaongea naye akaniambia wewe ni mtu tajiri.

“Alitaka tuongee aidha Kiingereza au Kiswahili na mimi nilimwambia bora tuongee Kiswahili, lakini aliniambia tuongee Kiingereza kwa kuwa ninaonekana kukizungumza vizuri.

“Aliniuliza wewe ni mtu tajiri utanipa shilingi ngapi, nilimwambia yeye ndiye aseme wanataka shilingi ngapi, hiyo ilikuwa siku ya kwanza ambayo ni Alhamisi,” alisema.

Alisema kuw amuda wote alikuwa ana tumaini kuwa atatoka, lakini siku zilikwenda na ilipofika Jumatano ya wiki iliyofuata, watekaji walimpigia tena simu ambapo aliwaeleza kuwa ni vyema kwa kuwa amefungwa na hawezi kufanya lolote, amtafute mwanafamilia ili aongee naye na baadaye wapate wanachotaka ili wamwachie, kwa kuwa alikuwa na wakati mgumu sana.

“Unajua ukishafungwa macho, kuna mtu unaweza kumfunga kwenye chumba na kuwambia huwezi kutoka hapa, mwanadamu anaanza kuchanganyikiwa. Yeye yuko huru kutembea kwenye hicho chumba

“Frustration (kuchanganyikiwa) kwangu ilikuwa high (katika kiwango cha juu), kuna wakati walikuwa wakinitisha, wakiniwekea bunduki kichwani wakisema wataniua, ilifika mahali niliwaambia waniue, kwa sababu ilishafikia mahali nilishapata frustration kiasi kwamba nilishagive-up (nilishakata tama) na maisha,” alisema.

Kuhusu kikombozi

Alisema hadi anaachiwa, familia yake haikutoa kikombozi chochote kwa watekaji hao, kwa kuwa ilifikia hatua wenyewe wakawa wameshatofautiana.

“Nikwambie ukweli kwamba sisi familia haijatoa pesa yoyote. Kwa sababu familia ingepata kujua kuwa bado Mohamed yupo, sasa watajuaje kuwa yupo, kwanza labda waongee na mimi na pili wangeweza kumuuliza yule mtekaji, muulize Mohamed hiki na hiki, akijibu tutajua kwamba huyo mtu bado yuko hai

“Lakini ukweli ni kwamba siku waliyoniachia sisi hatukutoa pesa yoyote. Iwapo wangelipwa kikombozi ningesema ukweli na kwamba kwa imani yangu, ninathibitisha kuwa hatujalipa kikombozi,” alisema.

Deni kwa Watanzania

Mo alisema ana deni kwa Watanznaia kutokana na namna walivyopigania kukombolewa kwake kutoka mikononi mwa watekaji hao.

Alisema wakati wote akiwa mikononi mwa watekaji, mke wake alikusanya magazeti yote ya Tanzania mbayo yalipigania kuachiwa kwake.

“Unajua jambo likitokea duniani kote au kwenye nchi jambo likitokea utaona siku ya kwanza unawekwa ukurasa wa kwanza, siku ya pili ukurasa wa pili, siku ya tatu ukurasa wa tatu, siku ya nne na kadhalika watu wanasahau.

“Lakini kwa zile siku 10 zote, kila siku niliona watu walikuwa wananiulizia na walikuwa wananiweka kwenye ukurasa wa kwanza, wakiuliza Mohamed yuko wapi, Mohamed yuko wapi,” alisema.

Alisema anawashukuru pia Watanznaia kupitia mitandao ya kijamii ambao waliweka hashtag #bringbackourMo au #whereisMo.

“Niwashukuru sana sana walijitolea na kutumia muda wao kupaza sauti, kulikuwa na shinikizo kubwa sana kiasi kwamba inaonekana wale walioniteka walikuwa na mtu aliyekuwa akiwapa taarifa nini kinachoendelea,” alisema.

Alisema jambo la tatu ni kwamba Tanzania ina zaidi ya watu milioni 55 na tuna tofauti nyingi, zikiwemo za kikabila, yeye akiwa ni mtu wa Singida tena Mnyaturu, kuna Wakurya, kuna utofauti wa dini, wakristo na waislamu lakini wote bila kijali tofauti zao za kikabila, kidini na kiitikadi walimuombea.

“Watu waliniombea misikitimni, waliniombea makanisani. Lakini kuna suala la asili. Mtu anaweza kusema Mohamed si asili yetu kwa sababu anatoka uhindini, lakini Watanzania walikuja pamoja  bila kujali imani zao za kidini, vyama vyao na walikuja pamoja kuniombea,” alisema.

Aliwashukuru wana Simba na wana Yanga ambao walijitokeza kwa wingi ikionyesha kuwa pamoja na tofauti zao.

 “Nikwambie kitu kimoja, leo hii niko hapa mbele yako ni dua ya watu, Watanzania na watu duniani, kwa hiyo nikwambie kitu  kimoja kwamba nina  deni kubwa kwa nchi yangu.

“Kama ambavyo hata wewe unajua kuwa kuna mkakati wa Bill Gates na Warren Buffets, wa kuhamasisha utoaji, ambao hata mimi nimesaini kuwa nusu ya mali yangu nitagawa kusaidia watu.

“Hii ilikuwa kabla ya tukio hilo lakini hiyo imenipeleka mbali zaidi kuharakisha kusaidia kutoa ajira, kusaidia kwenye maeneo ya maji na afya, kwa hiyo mimi ninasema asilimia 99 ambazo nitatumia kusaidia, nitazitumia kwa nchi yangu ya Tanzania ambayo nina deni nayo,” alisisitiza.

Kuachiwa mikononi mwa watekaji

Alisema alipotekwa, yeye alikuwa hajui wanampeleka wapi, lakini nyumba aliyohifanyiwa ilikuwa ndani ndani sana kitendo kilichomshangaza kuwa kwenye dunia ya leo unaweza kuchukuliwa na kufichwa mahali usionekane.

Alisema siku ambayo walimwachia kwa kumpeleka na kumwacha kwenye eneo la Gymkana alijua kuwa wale watu walikuwa wanakwenda kumuua, kwa kuwa alikuwa anajua hawajapata pesa.

“Yaani nakwambia yule mtu ambaye alikuwa akimwona kuwa akili yake haikuwa sawasawa, ambaye mara zote alikuwa akiniwekea bunduki kichwani, akinitisha, aliponiambia ananipeleka akaniache nilimshawishi atulie kwa sababu nilijua anakwenda kuniua.

“Nilimsihi kuwa walale waangalie siku iliyofuata, kuwa tuangalie uwezekano wa familia yangu kuwapa fedha lakini alisema atanipeleka kwa sababu mabosi wake hawapokei simu zake. Alikuwana frustration (kuchanganyikiwa) fulani.

“Nilimwambia mimi ni mwislamu kwa hiyo hata akiniua basi asinitupe mbali, kwa kuwa kuna taratibu za kunizika, yaani nilijua wataniua.

“Lakini kwa bahati nzuri waliniacha pale mimi bado nikiwa nimefungwa macho, baada ya kufungua, japokuwa lilikuwa eneo ambalo natumia kucheza golf, na karibu na ofisini kwangu, lakini ilinichukua karibu dakika saba kutambua niko wapi.

“Ilikuwa ndiyo mara ya kwanza naona vitu na waliponifikisha hapo, mmoja aliyekuwa nyuma yangu ambaye alionekana kama mtu mzuri alikuwa mkristo, nilimsihi wasirudie kufanya mambo kama hayo,” alisema.

Alisema walipokuwa kwenye gari ndipo kwa mara ya kwanza alishikana mkono na mtu huyo na ndipo alipoanza kuwa na tumaini kuwa hawatamuua.

Alisema waliopfika Gymkana walimsukuma, akawa amesimama na baadaye alisikia gari limeondoka.

Alisema baada ya muda alijifungua kamba alizokuwa amefungwaa baada ya muda alitambua yupo gymkana na kisha akatembea Southern sun

Alisema walipokuwa wakitoka kwenye nyumba ambayo alikuwa amefichwa, gari liliwashwa karibu mara 17 likawa linagoma na yeye kuwataka watekaji wamwachie  hapo nje ambapo walimjibu wakifanya hivyo polisi watawaua.

Alisema baada ya gari kuwaka alisikia harufu ya petroli, na wote walikuwa wakaivuta sigara wakati wakiwa kwenye nyumba alipofichwa na siku alipokuwa wakimuondoa walimkataza kuvuta kwasababu ndani ya gari kulikuwa na petroli.

Alisema baada ya kushushwa kwenye gari, alipofika eneo la ubalozo wa Umoja wa Ulaya (EU), alimuona askari anayelinda maeneo hayo lakini hakumtambua kwasababu alikuwa hajanyoa ndevu, kajifunga na kitambaa kama aulo ambapo ilikuwa kama yupo nusu uchi.

Alisema baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni Mo walimsaidia kumfikisha katika hoteli ya Southern Sun.

Hata hivyo alisema awali alikuwa akiogopa watu aliokuwa akionana nao njiani akihofia wanaweza kuwa watekaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles