Yanga mambo shwari Misri

0
772

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Yanga kilitua salama jana nchini Misri na kuendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids, unaotarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa June 30 nchini humo.

Msafara wa Yanga uliondoka juzi jijini Dar es Salaam, ukiwa na kikosi cha wachezaji 20, ambao watawavaa Waarabu hao ambao mchezo wa kwanza walishinda mabao 2-1, Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Ili  Wanajangwani hao waweze kuibwaga Pyramids wanatakiwa kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela, alisema wachezaji wao wote wapo vizuri  wakiwa na morali ya juu ya kutaka kupindua meza.

“Tulifika salama na wachezaji wanaendelea na mazoezi leo (jana) jioni kujiandaa na mchezo huu, hali ya hewa ya huku ni joto hivyo hakuna tofauti sana na nyumbani,” alisema.

Alisema hakuna figisu zozote walizofanyiwa tangu walipotua nchini humo.

“Kila kitu kinaenda sawa, hakuna figisu , tunachosubiri siku ifike tupambabe na inshallah tutashinda,”alisema.

Mwakalebela alisema bechi lao la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera linahakikisha maandalizi yote ya msingi yanaenda sawa.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini nafasi ya kufanya vizuri ipo, Watanzania wazidi kutuombea,”alisema Mwakalebela ambaye ni Katibu Mkuu wa zamani wa TFF.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here