24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani CCM washindwa kusoma kiapo

NA VICTOR BARIETY, GEITA

KATIKA hali ya kushangaza Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita juzi liligeuka kituko baada ya madiwani wanne kati ya 49 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kusoma kiapo kwa ufasaha.

Hali hiyo ilisababisha vicheko kutawala katika ukumbi wa halmashauri walimokuwa wanaapishwa madiwani hao.

Tukio hilo lilitokea saa 11:32 asubuhi muda mfupi baada ya mwenyekiti wa muda wa kikao hicho, Gaspar Kanyairita kufungua na hakimu mkazi, Joseph Wiliam kuanza zoezi la kuwaapisha madiwani hao.

Madiwani walioshindwa kusoma kiapo na kata zao kwenye mabano ni Heche Mathias (Nyakagomba), Khadija Joseph (Nyamigota), Daud Simeo (Nyamboge) na Sele Juma Isene (Nyamwilolelwa).

Mkuu wa wilaya ya Geita, Omari Mangochie na Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma hawakuweza kuvumilia hali hiyo na kujikuta wakiangua kicheko cha nguvu ambacho pia kilipokewa na wageni waalikwa na kusababisha ukumbi mzima kuzizima kwa kicheko wakati Diwani wa Kata ya Nyamboge akiapa kwa tabu mithili ya mwanafunzi wa shule ya awali.

Kutokana na hali hiyo, zoezi hilo la uapishwaji lilichukua muda mrefu kukamilika huku ukumbi mzima ukizidi kuzizima kwa vicheko.

Baadhi ya wananchi walishangazwa na hatua hiyo, ambapo mmoja wao alisikika akisema kutokana na baadhi ya madiwani kutokujua kusoma na kuandika kutazorotesha maendeleo yao.

“Kama diwani hajui kusoma hivi hapa wananchi waliomchagua watarajie maendeleo kweli au ndiyo wamejikaanga kwa mafuta yao…diwani kama huyu (anamtaja) anawezaje kukwepa kupitisha mikataba mibovu…hakika hii ni kali,’’ alisikika mwananchi mmoja aliyekuja kushuhudia viapo vya madiwani hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles