27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Mbarawa atoa maagizo Dawasco

mbarawaNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amelitaka Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), kufikisha maji kwa wateja milioni moja hadi kufikia Juni mwaka ujao.

Mbarawa alimtaka Mkurugenzi wa Dawasco, Cyprian Luhemeja kuongeza makadirio waliyokuwa wamejiwekea kwa kuongeza wateja kutoka  148,000 waliopo kwenye bili hadi kufikia milioni moja.

Profesa Mbarawa aliyasema hayo jana katika ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo mwishoni mwa wiki ambapo alisema uzalishaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam unategemea mitambo ya Ruvu Juu, Ruvu Chini pamoja na ule wa Mtoni.

“Naamini pindi tutakapofanya mazungumzo ya kina tutafikisha kiasi hicho cha wateja hiyo Juni mwakani na hilo mtalipima kwenye tathimini tutakapokutana Februari,” alisema Profesa Mbarawa.

Katika hatua nyingine waziri huyo alitoa wito kwa Dawasco kuanza mchakato wa kutumia mita za mfumo wa kulipia kabla kama inavyofanyika kwa simu na umeme.

“Njia hii naamini itasaidia kuwabana wakwepaji wa kulipa na hivyo kusaidia Dawasco kujipatia mapato ya kutosha,” alisema Mbarawa.

Alitoa wito kwa Mkurugenzi wa Dawasa, Archard Mutalemwa kuhakikisha  wanaweka miundombinu bora ili kuokoa upotevu wa maji ili kuboresha  huduma ya kuongezeka kwa wateja walio kwenye mfumo wa bili watakaofikia milioni moja.

Akizungumzia kuhusu mipango yao, Mkurugenzi wa Dawasco, Luhemeja alisema wanaamini idadi hiyo itafikiwa huku akisema hadi sasa katika jiji la Dar es Salaam wateja wamefikia asilimia 68 wanaopata maji kwa uhakika.

Alisema hadi kufikia Februari wataweza kuvuna maji mengi kutoka mita za ujazo 300,000 hadi kufikia mita za ujazo 756,000 zitakazohudumia wateja wapya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles