26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mabasi kuanza safari saa 11 alfajiri Des. 20

LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

MABASI ya abiria yanayofanya safari kwenda mikoani na nchi jirani, yanatarajia kuanza safari saa 11:00 alfajiri katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki Mabasi Tanzania (Taboa), Enea Mrutu aliliambia MTANZANIA jana kuwa hatua hiyo ilifikiwa katika kikao kati yao, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.

Mrutu alisema utaratibu huo utayahusu mabasi yanayokwenda mikoa yote nchini isipokuwa katika maeneo yenye changamoto kubwaya kiusalama ikiwamo Kigoma, Sumbawanga na Rukwa.

Alisema utaratibu huo utaanza kutekelezwa Desemba 20 mwaka huu, ambapo magari yote yaliyokuwa yakizuiwa Dodoma, Morogoro na Shinyanga sasa yataruhusiwa kutembea usiku ili yakamilishe safari.

“Kwa mfano njia ya kati sehemu yenye changamoto ni kutoka Shinyanga kwenda Mwanza, hapo tumekubaliana uwekwe utaratibu kwamba kwa sababu magari ni mengi yawe yanasimamishwa, yakifika 10yanapewa ‘escort’ ya polisi yanakwenda.

“Kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam shida kubwa hapa ni malori, tumependekeza ikifika saa 4:00 usiku malori yazuiwe hadisaa 7:00 au 8:00 usiku ili kupisha mabasi yatembee, ili tuone matokeo katikakipindi hiki chote cha sikukuu,” alisema Mrutu.

Alisema ili kuhakikisha usalama wakati wotewa safari, Sumatra inapaswa kuhakikisha mabasi yote yatakayoruhusiwa kutembea usiku yawe yameunganishiwa mfumo maalumu wa ulinzi (GPS) ili yaweze kuonekana kwenye mfumo wa mamlaka hiyo.

Alisema kama chama wanaamini mfumo huo ndio shuluhisho sahihi la ajali kutokana na uchunguzi walioufanya tangu kuanza kutumika mwishoni mwa mwaka 2016.

“Speed governor’ ilianza kutumika mwaka 1995,tochi zikaja 2013 hadi 2016, ajali zilizotokea tunazifahamu kwa sababu wote tulizishuhudia, mwishoni mwa mwaka huo tukaja na GPS ambayo sisi tunaamini imepunguza ajali, hata inapotokea madhara yake yanakuwa madogo.

“Ukiacha ile ya Igunga ya basi la City Boyambayo lori liliangukia, nyingine zote madhara yamekuwa madogo. Kama unakumbuka ajali ya lile basi lililoua watu wengi Mbeya na ile Hiace zote hazikufungwa GPS,”alisema Mrutu.

Wakati huo huo, Mrutu alisema wamepata taarifa ya kuanza ujenzi wa jengo kubwa la kibiashara katika eneo la Stendi Kuu ya Mabasi ya Ubungo jijini Dar es Salaam, unaotarajiwa kutekelezwa na kampuni moja ya kichina huku wakiwa hawajapokea taarifa rasmi kutoka halmashauri ya jiji hilo.

Mrutu alisema walipata taarifa hizo baada ya kutembelea katika jengo maarufu la Ubungo Plaza na kukuta mchoro wa jengo hilona baadaye kuelezwa na mtu mmoja ambaye hakumtaja kwa jina kuwa ujenzi huoutaanza mwezi huu.

“Kama taarifa hizi ni za kweli maana yake ni kwamba tutatakiwa kupisha ujenzi kwa sababu ujenzi hauwezi kufanyika tukiwa ndani. Inamaanisha lazima twende Mbezi ambako hatujaona kama wameanza maandalizi yoyoye.

“Sisi tulijua kuwa Halmashauri ya Jiji haijapata fedha, lakini tumeshtushwa na kauli ya Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo hivi karibuni kuwa fedha zilikwishatolewa, sasa tunachojiuliza ni kwamba kwanini halmashauri wasitueleze wakati tunafanya nao kila siku na ujenzi nisuala la muda mrefu,” alisema Mrutu.

Alisema msimamo wao ni kwamba hawawezi kuhamia huko endapo maandalizi ya kutosha hayajafanyika ili yasiwatokee yakeyaliyotokea baada ya kuhamishwa kwa stendi kuu ya mabasi jijini Dodoma.

Vile vile Taboa imekemea tabia ya baadhi ya taasisi za kiraia ambazo hutumia sikukuu za mwisho wa mwaka kufanya ukaguzi wa magari kinyume cha utaratibu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles