Apandishwa kizimbani kwa unyang’anyi wa kutumia silaha

0
1092

AVELINE KITOMARY NA JOHN KIMWERI (DSJ) -DAR ES SALAAM

MKAZI wa Kigogo Kati, KulwaAlly (33) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni mwishoni mwa wiki kwa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisomewa shtaka hilo mbele ya hakimu Joyce Mushi, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Ramadhan Mkimboalidai kuwa Machi 30, mwaka huu eneo la Magomeni Morocco, Wilaya ya Kinondoni,Dar es Salaam, mshtakiwa alimtishia Mwinyipembe Waziri kwa panga na kuiba pikipiki aina ya Boxer yenye namba MC 538 yenye thamani ya Sh 2,360,000 mali yaFatuma Miraji.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo, huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana mshtakiwa alirudishwa rumande hadi itakaposomwa Desemba 28,mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here