30.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yaipiga jeki ujenzi Hospitali Muheza

Susan Uhinga, Muheza

Benki ya NMB imekabidhi mabati yenye thamani ya Sh milioni tano kwa uongozi wa Wilaya ya Muheza kusaidia ujenzi wa Hospitali ya wilaya.

Akikabidhi msaada huo wa mabati 229 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Cosmas Gabriel, amesema mbali na huduma wanazozitoa pia wameona kuna umuhimu wa kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua kero zinazowakabili wananchi.

“Sisi NMB tumeguswa kutokana na umuhimu wa huduma za afya lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya na za uhakika.

“Kwa kuzingatia pia mabati hayo yataenda kutumika katika jengo la wodi ya kina mama kwa ajili ya huduma ya afya ya mama na mtoto kwao ni jambo la faraja kwa kuwa wanawake ndiyo wadau wakubwa wa maendeleo,” amesema.

Mabati hayo yameombwa na umoja wa wanawake wilaya ya Muheza kwa Benki ya NMB lengo likiwa kupata mabati ya kuhezekea jengo la kina mama.

Akipokea mabati hayo Katibu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), Mkoa wa Tanga, Sophia Mkupe, ameishukuru benki hiyo na kusema kwamba wadau wengine waige mfano kutoka kwa benki hiyo katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.

“Wazo la kuwa na Hospitali ya Wilaya liliibuliwa na wanawake wa Wilaya ya Muheza kutokana na changamoto wanazokutana nazo katika kupata huduma za afya ya mama na mtoto,” amesema.

Aidha, Mkupe ameutaka uongozi wa benki ya NMB kuangalia namna bora ya kupunguza riba na masharti ya upatikanaji wa mikopo ili wanawake waweze kunufaika na mikopo itolewayo na benki hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles