Maalim Seif atimkia ACT-Wazalendo

Na Nora Damian

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad, amesema ameamua kujiunga na Chama cha ACT – Wazalendo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika zilizokuwa ofisi za wabunge wa Cuf Magomeni, amesema mapambano ya kisiasa lazima yaendelee.

“Mapambano ya kujenga demokrasia na kusimamisha utawala wa haki unaoheshimu sheria si kazi lelemama.

“Tumefanya kazi kubwa mpaka hapa tulipofikia ni jukumu letu sasa kuikamilisha kazi hiyo, tunahitaji jahazi la kutufikisha kwenye Tanzania mpya inayoheshimu utu, ubinadamu, haki na neema inayofikia wananchi wote na jahazi hilo ni ACT – Wazalendo,” amesema Maalim Seif.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here