25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

DC Pangani: Hata mimi nikibainika kuhusika na magendo nitaachia ngazi

Oscar Assenga, Pangani

MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga, Zainabu Abdallah amesema wote wanaohusika na biashara haramu za magendo wilayani humo watachukuliwa hatua kali za kisheria na pia kwa viongozi watawaondolewa kwenye nafasi zao na kama naye atabainika kuhusika na hayo ataachia ngazi.

Mkuu huyo wa wilaya alitangaza hayo wakati wa kikao cha pamoja baina yake na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo wakiwemo madiwani, wenyeviti na watendaji wa kata na vjiji ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupambana na biashara haramu za magendo wilayani humo.

Alisema haiwezekani viongozi wakawa wanashirikiana na wafanyabiashara kupitisha bidhaa za magendo na wao kuendelea kufumbia macho jambo ambalo linaleta athari kubwa kwa uchumi wa wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.

“Labda niwaambia kwamba uwe Mwenyekiti wa Kijiji, Watendaji wa Vijiji na Kata ikibainika umehusika kupitisha bidhaa za magendo utupishe ukae pembeni na ukatafute kazi nyengine za kufanya,“ amesema DC Zainabu.

“Lakini pia tuna taarifa kwamba wapo watu wanapokea mishahara miwili kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa ili wawape taarifa za siku tunazoweka ulinzi na mitego mbalimbali ili kuwabaini siku zao zinahesabika maana hawatapona kwenye vita hii,“ ameeleza.

Aidha alisema pia pamoja na kwamba vita hiyo ni ngumu lakini wataweka mikakati imara kuweza kukabiliana nayo kwa lengo la kuhakikisha inaondoka kwenye maeneo yao .

 “Pia nyumba zinazotumika kuhifadhi bidhaa za magendo nazo tutazikamata na wahusika wake tutwafikisha mahakamani kujibu tuhuma ambazo zinawakabili za kujihusisha mambo hayo,“ ameeleza DC Zainabu.

Naye Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama amesema kupitisha mizigo kwenye bandaru bubu ni kuvunja sheria za nchi namba 17 ya 2004 na kifungu 47 ambacho kinaelekeza mizigo au abiria watashuka au kupakia eneo lilorasmi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles