28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Lwandamina si mtu wa mchezo mchezo

Kaimu Katibu Mkuu wa mashabiki wa Klabu ya Zesco United, Elias Kangwa, akimkabidhi zawadi ya saa Kocha George Lwandamina, wakati wa hafl a ya kumuagakocha huyo aliejiuzulu juzi.
Kaimu Katibu Mkuu wa mashabiki wa Klabu ya Zesco United, Elias Kangwa, akimkabidhi zawadi ya saa Kocha George Lwandamina, wakati wa hafl a ya kumuagakocha huyo aliejiuzulu juzi.

* Anapiga hadi ngumi, watovu wa nidhamu Yanga kukiona

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KAMA wachezaji wa Yanga wanaamini kuondoka kwa Hans van der Pluijm kutawapa nafasi ya kufanya mambo watakavyo, basi wamekosea maana huyo George Lwandamina si mtu wa mchezo mchezo hata kidogo.

Inadaiwa kocha mpya mtarajiwa wa Yanga ambaye ni Mzambia, ukimzingua anapiga hadi ngumi.

Wachezaji wa Yanga mara kadhaa wamekuwa wakisikika kumlalamikia Mholanzi Pluijm ni mkali na yupo makini wakati wote katika kusimamia nidhamu.

Sasa hivi watakutana na mkono wa nidhamu wa Lwandamina, ambaye kufuatia kujiuzulu kwake Zesco United, kocha huyo atatua Yanga na taarifa zinadai atawasili nchini leo kuifundisha klabu hiyo kongwe nchini.

Ujio wake ni ujumbe tosha kwa wachezaji wa Yanga kukaa mguu sawa, kwani mchezaji hata kama ukiwa mzuri ila una nidhamu mbovu hatakupanga kwenye timu mpaka ujirekebishe, lakini si kwa wachezaji tu hata viongozi Yanga wakae sawa kwani si mtu wa kupelekwapelekwa ana misimamo mikali.

Lwandamina juzi alijipa nafasi kukutana na wachezaji wa Zesco United na kuwaaga baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu yenye mafanikio ikiwemo kuifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali Klabu Bingwa Afrika mwaka huu.

Taarifa kutoka klabu ya Zesco United zinadai wachezaji wa klabu hiyo walifurahia na kushangilia taarifa za kuondoka kwa kocha huyo wakijiona wametoka kifungoni.

“Ni kweli Lwandamina mkali sana, wachezaji walifurahia sana baada ya kuagwa na kocha wao, ila amewataka kuendeleza nidhamu aliyoiacha,” kilieleza chanzo ndani ya Zesco United.

MTANZANIA liliwasiliana na Juma Luizio, anayecheza soka la kulipwa katika klabu hiyo ambaye alikiri kuwepo kwa shangwe kwa wachezaji wenzake baada ya kuagwa rasmi na Lwandamina.

“Lwandamina alikua mkali sana, ni mtu mwenye msimamo na hataki ujinga, nawajua wachezaji wetu wa Tanzania na huu ni wakati sasa wa wachezaji Yanga kuwa makini na kocha huyu.

“Nawashauri kufuata maagizo na kile anachotaka la sivyo watamwona mbaya, yeye huwa hajali kuonekana hivyo ni mtu muwazi na aliyenyooka na misimamo yake, naitarajia Yanga nyingine kutokana na ujio wa kocha Lwandamina,” alisema Luizio.

Nao mashabiki wa Zesco United waliandaa tafrija fupi ya kumuaga kocha wao wakimmiminia sifa kwa mafanikio aliyoiletea klabu na ushirikiano aliouonyesha kwa mashabiki.

Kaimu Katibu Mkuu wa Mashabiki wa Zesco United, Elias Kangwa, alisema wanabariki maamuzi ya Lwandamina maarufu kama Chicken (Kuku) kuondoka kujiendeleza katika kazi yake ya ukocha.

“Tunapenda kukushukuru kwa kazi nzuri uliyoifanyika Zesco United na tumejifunza mambo mengi kuhusu michezo kupitia wewe kwani hata wakati tulipokuwa tunakushutumu bado uliendelea kutuheshimu,” alisema Kangwa.

Lwandamina alisema hajawahi kucheza soka la kulipwa enzi zake za uchezaji na sasa ni nafasi yake kwenda kujifunza namna watu wengine wanavyofanya vitu huku akiwa na matumaini siku moja atarudi Zesci United akiwa na ujuzi zaidi.

Kocha huyo anayetarajiwa kutua Yanga, alikabidhiwa saa kama kumbukumbu ya kazi nzuri aliyoifanyia Zesco United.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles