Mabeste: Bila mke mimi si chochote

0
1336

11863462_824330024332919_8032859196560071225_n

NA BEATRICE KAIZA

MSANII wa Hip Hop nchini, William Ngwi ‘Mabeste’, ameweka wazi kwamba mke wake, Lisa Fickenscher, ndiye mwongozo wa maisha yake kwa ujumla.

Akizungumza na MTANZANIA, Mabeste alisema mkewe amekuwa na upeo mkubwa unaomwongoza katika ushauri wa maisha yao na watoto wao.

“Mke wangu ni kiongozi shupavu mwenye upeo Mkubwa, nadiriki kusema kwamba bila yeye mimi si chochote katika maisha yetu,” alieleza Mabeste.

Wawili hao wanaoshirikiana pia katika kazi ya muziki wapo katika maandalizi ya kupata mtoto mwingine, huku wakijinadi kufanya kazi kwa bidii ili kuwatengenezea maisha mazuri watoto wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here