23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ibrahimovic awaomba radhi mashabiki Man United

Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic

MANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI hatari wa klabu ya Man United, Zlatan Ibrahimovic, amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya mchezaji huyo kusimamishwa mchezo mmoja.

Mchezaji huyo amepewa adhabu ya kusimamishwa mchezo mmoja, baada ya kuoneshwa kadi tano za njano katika msimu huu, hivyo kumfanya akose mchezo mmoja.

Ibrahimovic alioneshwa kadi ya njano katika mchezo ambao ulipigwa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Swansea City, huku timu yake ikiondoka na ushindi wa mabao 3-1.

Manchester United inatarajia kushuka dimbani Novemba 19 dhidi ya Arsenal, hivyo mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kutokana na kuitumikia kadi hiyo ya njano.

Kutokana na hali hiyo, Ibrahimovic amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kuukosa mchezo muhimu kwa klabu yake mara baada ya kumalizika kwa michezo ya kimataifa.

“Naomba radhi kwa mashabiki wa Man United, nimesimamishwa mchezo ujao kutokana na kuoneshwa jumla ya kadi tano za njano msimu huu.

“Siamini kwa kilichotokea, ukweli ni kwamba nilikuwa na lengo la kutaka kucheza dhidi ya Arsenal, lakini baada ya kuoneshwa kadi hiyo siwezi kucheza mchezo huo.

“Lakini ninawaamini wachezaji wenzangu kuwa wanaweza kufanya makubwa zaidi katika mchezo huo na kuibuka na ushindi bila ya mimi kuwepo uwanjani.

“Kila wakati najaribu kucheza kwa kutumia nguvu, lakini nashangaa kwamba ninaonekana kuwa ninacheza vibaya na kuoneshwa kadi za njano.

“Sijui niseme nini juu ya hali hii, naweza kusema kuwa nimechoka na mambo ambayo wananifanyia waamuzi.

“Soka la nchini England linahitaji mchezaji kutumia nguvu, ni lazima nikubaliane na hali hiyo,” alisema Ibrahimovic.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo amedai kuwa wapo wachezaji wengi ambao wanacheza kwa kutumia nguvu, lakini waamuzi hawafanyi lolote kwa wachezaji hao, ila kwa upande wake wamekuwa wakimfuatilia sana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles