23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Lukuvi ataka NMB, NHC waunganishe nguvu


NA MWAMDISHI WETU-ARUSHA

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametoa wito kwa Benki ya NMB kuungana na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), ili kusaidia utatuzi wa changamoto ya umiliki wa nyumba bora na za kisasa miongoni mwa Watanzania.

Lukuvi ametoa wito huo wakati wa uzinduzi wa NMB Nyumba Day Expo 2019, unaolenga kuwakutanisha wadau wa sekta ya ujenzi na kutoa elimu na uelewa kwa wananchi juu ya mikopo ya nyumba na namna sahihi ya kumiliki nyumba bora.

Alisema kumekuwa na changamoto kubwa kwa Watanzania wa kada mbalimbali katika kumiliki viwanja, kupata hati za viwanja hivyo pamoja na vibali vya ujenzi na kwamba ushirikiano wa kikazi baina ya NMB na NHC, utasaidia kumaliza changamoto hiyo.

Kupitia maonyesho hayo yanayofanyika jijini Arusha, Waziri Lukuvi alibainisha kuwa Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 421 kwa taasisi za fedha nchini kupitia Sheria ya Fedha za Mikopo ya Makazi ya Mwaka 2008, kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwezesha upatikanaji wa makazi ya kutosha.

Awali akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho hayo, Mkuu wa Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB, Salie Mlay, aliahidi kuufanyia kazi wito wa Waziri Lukuvi, huku akibainisha kuwa katika kipindi cha miaka miwili, wametoa mikobo ya zaidi ya Sh bilioni 17.

Mlay alibainisha kuwa mikopo hiyo imetolewa kwa zaidi ya wateja 139 kote nchini, huku akiahidi kuwa Benki yake kwa kushirikiana na NHC watajikita katika kuwawezesha wananchi wa Arusha kumiliki viwanja na nyumba kwa gharama.

Aliongeza ya kwamba, kwa kuanzia watahakikisha wakazi wa Arusha wanamiliki viwanja na kupata makazi kwa gharama nafuu katika mradi wa ujenzi wa makazi wa Safari City, unaofanyika huko Mateves, nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Mlay alisisitiza ya kwamba, benki yake kupitia NMB Mortgage Finance imejikita katika kufanikisha hilo kwa lengo la kuwezesha wateja kumiliki makazi bora na nafuu, kulingana na kasi ya ongezeko la watu mijini na vijijini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles