20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Mbaroni kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake

Na HARRIETH MANDARI-GEITA

JESHI  la Polisi mkoani Geita linamshikilia mkazi wa Kata ya Nyankumbu, Selemani Mathis (35), kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka minne.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo, alisema mtuhumiwa huyo yuko rumande akisubiri uchunguzi tuhuma dhidi yake ukamilike ili aweze kufikishwa mahakamani.

Alisema Siku ya tukio, mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi na baba yake baada ya mama yake kutengana na baba yake na kumwacha mtoto huyo na mdogo wake wa miaka miwili.

“Siku ambayo unyama huo ulipofanyika mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto wa jirani na baada ya kucheza walikwenda nyumbani kwa hao majirani na ndipo mtoto wa mama wa jirani huyo alipomwambia mama yake kuwa rafiki yake alikuwa anajikuna kila wakati sehemu za siri,” alisema Kamanada Mponjoli.

Alisema baada ya mama huyo wa jirani kusikia hivyo alimwita mtoto huyo na kuanza kumuhoji kwa nini anajikuna na ndipo mtoto huyo alipeeleza jinsi baba yake alivyomuingilia.

“Hatutapenda kumtaja jina huyu mama jirani kwa kuwa anatusaidia upelelezi na alifafanua kuwa  mtoto huyo alisema mara baada ya kumbaka baba huyo alimtishia kumuua iwapo atatoa siri hiyo kwa watu,”alisema.

Ilidaiwa kuwa kutokana na kuwepo kwa mgogoro kati ya wazazi hao, mama wa watoto hao aliamua kuhama nyumbani hapo na kuwaacha watoto wakilelewa na baba yao pekee hali ambayo ilionekana kuchangia kutendeka kwa unyama huo.

“Hebu nyie wakina mama angalieni sana mnapogombana na waume zenu msiwaache watoto hasa wakiwa wadogo namna hii mnawasababishia madhara makubwa sana hasa ya ukiukwaji wa haki za binadamu kama haya,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles