24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Shaka: Bila ujasiri wa Karume Muungano ungekawia

Na MWANDISHI WETU-MOROGORO

IMEELEZWA kuwa jamii ya Watanzania hawataacha kusahau katika suala la kumuenzi, kumuheshimu na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa katika taifa na Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume.

Hatua hiyo inamtaja kuwa ndiye kiongozi pekee aliyekuwa na uthubutu wa kuiunganisha nchi yake na kuunda Jamhuri moja ya Muungano na kuzaliwa kwa Taifa jipya la Tanzania.

“Maisha ya Sheikh Karume kushiriki kwake siasa, kutumia muda mwingi kukijenga chama cha ASP hadi kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar na kupatikana ukombozi kamili wa waafrika  Zanzibar, kuna mchango mkubwa wa hekima, busara na ujasiri wa kiongozi huyo, daima milele tutaendelea kumuenzi sheikh Karume, kujifunza kutokana na ushupavu wake lakini pia maono yake ya mbali katika kupigania maendeleo na usawa wa kila  mtu,” alisema Shaka.

Hayo yalisemwa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza kuhusu kumbukizi ya miaka 47 ya kifo cha Mzee Abeid Amani Karume ambapo alimtaja kiongozi  huyo kwamba alikuwa shujaa, mzalendo, mpigania haki na mpenda umoja wa Afrika na watu wake.

Shaka alikumbusha kuwa Sheikh Karume ndiye aliyemwambia Mwalimu Nyerere tuungane haraka na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere awe Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo  lilihitaji ujabali, ujasiri na uzalendo wa kutosha  ili kufikia maamuzi magumu ambayo yanakwenda kulijenga na kulimairisha Taifa bila ya tamaa ya aina yoyote.

“Walipokubaliana kuziunganisha nchi zao mbili huru , Mzee Karume hakutaka longolongo, alimueleza Mwalimu Nyerere tukawaulize wananchi ili tuungane, akasema Rais wa kwanza wa muungano uwe wewe Mwalimu Nyerere, uamuzi huu viongozi wengi Afrika uliwaishinda kwa tamaa ya madaraka,” alisema Shaka Alisema kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kwa sasa ni kuendelea  kuamini kuwa kilichokufa mwaka 1972 ni kiwiliwili cha Sheikh Karume bali fikra na mema yote alioyaanzisha katika uhai wake yanadumishwa kinadharia na vitendo na  siku zote tuendelee kuamini kuwa njia pekee yenye heshima, utii na upendo ni  kuyatetea mapinduzi ya Zanzibar ya Januari  1964  na kuilinda misingi ya Muungano

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles