27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

 LIPUMBA  ASIKITISHWA UMASKINI KWA WANANCHI

Na CLARA MATIMO, MWANZA


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, ameishangaa serikali kwa kujinadi kwamba uchumi wa nchi unakuwa  kwa  asilimia 7.1 wakati wananchi  wengi bado  ni maskini.

Alikuwa akizungumza  jijini hapa juzi katika kongamano la vijana wa chama hicho lililowahusisha  vijana kutoka wilaya za Ilemela na Nyamagana mkoani Mwanza.

Profesa Lipumba alisema  serikali imeshindwa kukopa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania ili kuwakopesha wananchi waweze kupata mitaji ya kufanyia biashara.

Alisema  kitendo cha  serikali kuingiza katika bajeti baadhi ya miradi ambayo haikupitishwa na bunge kinayumbisha uchimu wa nchi.

“Hali hii inavuruga utaratibu mzima wa fedha za maendeleo ambazo hupitishwa na bunge kwa ajili ya shughuli mbalimbali ndiyo maana uchumi wa nchi unayumba.

“Huwezi kusema uchumi unakuwa wakati wananchi wako wengi wanamaisha duni na ni masikini,”alisema Lipumba.

Akizungumzia  uchumi wa viwanda, Profesa Lipumba alisema  ni sharti serikali iwezeshe wakulima kulima kilimo cha kutumia trekta badala ya jembe la mkono.

Alisema  viwanda  vinavyotakiwa kuanzishwa vitokane  na mazao ya wakulima yakiwamo pamba, chai, kahawa na  korosho.

Kuhusu demokrasia  nchini, alisema  kwa sasa nchi haiendeshwi kwa demokrasia bali inaendeshwa na  kundi la watu au mtu mmoja mmoja ambaye hataki kukosolewa kwa malumbano ya hoja.

Alishauri  ziundwe asasi ambazo zitasimamia utawala bora.

Akizungumzia  ustawi wa jamii, alisema  bado kina mama wajawazito hawapati lishe bora wakati wa ujauzito ndiyo sababu wengi wao wanajifungua watoto wanakufa na wengine wana utapiamlo.

Profesa Lipumba alisema  CUF itamaliza tatizo hilo itakapoingia madarakani mwaka 2020 kwa kuwa imejipanga kushika dola.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles