24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

LEMA: JPM INGILIA KESI YA WAKILI MWALE

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemwomba Rais Dk. John Magufuli, aingilie kati suala la Wakili Median Mwale, ambaye amekaa mahabusu kwa zaidi ya miaka sita bila kesi yake kuamuliwa.

Mwale na wenzake Donbosco Gichana (Raia wa Kenya), Boniface Mwimbwa na Elieas Ndejembi walikuwa wanakabiliwa na mashitaka 44 tofauti ikiwemo la utakatishaji fedha, kughushi nyaraka na kukutwa na mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu.

Hata hivyo mwishoni mwa Oktoba mwaka huu, Mahakama Kuu ya Arusha iliwaachia huru washtakiwa hao lakini walipotoka nje walikamatwa na kurejeshwa magereza.

Siku chache baadaye walifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha na kusomewa upya mashitaka 42.

Akizungumza jana, Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, alisema kitendo cha kumweka mtu mahabusu kwa muda mrefu bila kesi yake kuamriwa ni sawa na ukatili.

“Inauma sana kwamba ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka) na mahakama, kwa zaidi ya miaka sita wameshindwa kumaliza shauri hili.

“Kumweka mtu mahabusu kwa miaka yote hii ni ukatili mbaya sana, kwa kipindi ambacho nimekuwa gerezani nimeweza kuelewa huzuni za familia na watuhumiwa.

“Ndio sababu wakati Rais alipowasamehe wafungwa hasa wenye makosa makubwa nilimshukuru sana kwa sababu najua huzuni ya kukosa uhuru,” alisema Lema.

Alisema ni muhimu watu wote walioko kwenye vyombo vya sheria wajue kwamba wajibu wao unapokosa utu na upendo unaumiza watu kwa kuwatesa.

“DPP nguvu uliyopewa na sheria inapokosa upendo na haki basi inakuwa ni ukatili wa ajabu, ninamuomba mheshimiwa Rais aingilie kati suala la Wakili Mwale, kwa kweli huyu mtu inatosha kuwepo magereza kwa zaidi ya miaka sita bila kuhukumiwa,” alisema.

Wakili Medium Mwale na wenzake watatu, walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka 42 yakiwamo ya…

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako leo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles