25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WAZEE RORYA WALALAMIKA KUCHAPWA VIBIKO

NA SHOMARI BINDA-RORYA

WAZEE wa Wilaya ya Rorya mkoani Tarime, wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na vijana kwa kuchukua hatua ya kuwachapa viboko kwa kile kinachodaiwa kuendeleza mila potofu ambazo pia zimekuwa zikiwadhalilisha na kuendeleza ukatili.

Wakizungumza kwenye semina iliyoandaliwa na shirika la Masister wa Moyo Safi wa Maria Afrika na kuwashirikisha wazee wa mila wa wilaya hiyo katika kampeni ya kupambana na ukatili wa kijinsia, walisema maadili kwenye jamii yamepungua na ndiyo kunapelekea kuendelea kwa vitendo vya ukatili.

Walisema si wanawake pekee wanaofanyiwa ukatili bali hata wazee pia wamekuwa wakifanyiwa hivyo kwa kuendeleza mila za kuwachapa viboko pale wanapodaiwa kutenda kosa jambo ambalo wamedai linawadhalilisha na ni moja ya ukatili wanaofanyiwa.

Mmoja wa wazee hao aliyejitamulisha kwa jina la Andrecus Nyazam wa Kijiji cha Kwibuse, alisema zipo taratibu za kufuata pale mtu anapokuwa amekosa kwenye jamii lakini si vijana kuchukua hatua ya kuwachapa wazee viboko.

Alisema mila hiyo ni ya ukatili sawa na ule ambao wamekuwa wakifanyiwa wanawake kwenye jamii na kudai elimu bado inapaswa kuendelea kutolewa zaidi ili kuachana na mila ambazo zimekuwa kikwazo.

“Tunashukuru kwa semina hii ambayo tumeshirikishwa ili kwa pamoja tuweze kuimarisha haki za wanawake walioathiriwa na ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yetu lakini na sisi wazee tumekuwa na kilio chetu cha kudhalilishwa na kufanyiwa ukatili na vijana kwa kuchapwa viboko.

“Tunakwenda kutoa elimu kwa jamii juu ya kuachana na vitendo vya ukatili kwenye jamii zetu tunaomba pia sauti zisikike za kukemea mila zisizofaa ambazo kwa kiasi kikubwa ndio chanzo cha ukatili unaokuwa unatendeka,”alisema.

Mratibu wa mradi wa kuimarisha haki za wanawake walioathiriwa na ukatili wa kijinsia unaotekelezwa kwenye Kata 13 za Wilaya ya Rorya, Nollasko Mgimba, alisema jamii inapaswa kuweka mpango wa kutokomeza mila ambazo hazifai kwenye jamii.

“Pamoja na ukweli kwamba mila zina umuhimu wake mkubwa katika jamii, lakini tunapaswa kubadilika na kuachana na mila zisizofaa kulingana na maendeleo ya kijamii hasa katika nyanja za kiuchumi na kijamii,” alisema.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles