23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MFUMO WA ELEKTRONIKI KUTUMIKA BANDARINI

Na TUNU NASSOR

-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), imewataka wadau wa bandari nchini kuanza utumaji wa nyaraka kwa njia za kielektroniki ili kurahisisha uondoshaji wa mizigo.

Akizungumza na wadau hao juzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Sumatra, Gilliard Ngewe alisema baadhi ya wamiliki wa kampuni za meli wamekuwa hawatekelezi agizo hilo na hivyo kusababisha kuongeza gharama zisizo za lazima.

Alisema kuanzia jana wamiliki hao wanatakiwa kutumia njia za kielektroniki katika kutuma nyaraka za mizigo.

“Mnatakiwa kutumia njia za kielektroniki kutuma nyaraka kuanzia kesho(jana) ama sivyo nitawanyang’anya leseni za usajili,” alisema Ngewe.

Ngewe aliwataka pia wamiliki wa bandari kavu(ICDs) kuacha tabia za ucheleweshaji wa makusudi wa uondoshaji wa mizigo bandarini kwa nia ya kujipatia fedha zaidi.

“Mnatakiwa kusoma alama za nyakati ucheweji wa kwenda kutoa mizigo bandarini ili kuwaongezea gharama wateja muache mara moja kabla hatujawachukulia kali,” alisema Ngewe.

Awali Katibu wa Chama cha Mawakala wa Forodha(TAFFA), Tony Swai alilalamikia nyaraka kutokutolewa kwa njia ya kielektroniki huku wakitakiwa kulipa fedha kiasi cha Dola za marekani 45 kwa kila nyaraka wanayoihitaji katika kutoa mzigo.

“Upatikanaji wa nyaraka za mizigo unachukua kati ya siku mbili hadi nne huku ICDs nao wanakwenda kuutoa baada ya muda mrefu ili kutuongezea gharama mawakala hii inafanya wadau wengine kuikimbia bandari,” alisema Swai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles