30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

MALI ZA CCM KUNG’OA VIGOGO

Na NORA DAMIAN

-DAR ES SALAAM

TUME iliyoundwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. John Magufuli, kuchunguza mali za chama hicho nchi nzima tayari imeanza kazi, huku vigogo wanaodaiwa kujimilikisha mali wakijisali mbele ya tume hiyo.

Tume hiyo inayongozwa na Dk. Bashiri Ali, ilitangazwa iliundwa Desemba 20, mwaka huu na kutangazwa katika kikao cha kwanza cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, alisema kamati hiyo ilianza kufanya kazi tangu ilipoundwa.

“Hadidu za rejea wanazo wajumbe wa kamati lakini kazi kubwa ni kufuatilia mali za chama kokote ziliko. Tume kazi yake ni kwenda kuhakikisha kila mali inafahamika,” alisema Polepole.

Alisema pia wanachama wengi wameanza kujitokeza kutoa ushirikiano kwa kueleza namna wanavyozijua mali za chama na hata kutaja ziliko.

“Wanachama wengi wanatoa ushirikiano, wanaeleza wapi mali ziliko. Kwa viongozi na watumishi ni maelekezo kwamba watoe ushirikiano kwa tume,” alisema.

Katibu huyo alisema mali zote ni za wana CCM kupitia tume hiyo watarajie matokeo makubwa.

“Tunasema bodi ya wadhamini lakini wanufaika wakubwa ni wana CCM, mali za chama ni za wanachama,” alisema Polepole.

VIGOGO HATARINI

Kuanza kazi kwa tume hiyo huenda kukawaweka roho juu baadhi ya vigogo katika chama na serikali kufuatia maagizo yaliyotolewa na Rais Dk. Magufuli wakati anaunda tume hiyo.

Rais Magufuli alisema tume hiyo itafuatilia mali za chama hicho popote zilipo na itamhoji kila mtu anayehusika katika chama na Serikali.

“Mtakwenda kumhoji mtu yeyote, viongozi na watendaji wa CCM katika mikoa, wilaya, kata, matawi na mashina mtoe ushirikiano ili kuhakikisha mali za CCM hazipotei…

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako leo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles