25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM AANZA KUJITAMBULISHA KWA WANACCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Edmund Mndolwa (kulia), akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za CCM, Wilaya ya Korogwe. Pembeni ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Tanga, Jeingata Shedafa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Edmund Mndolwa  amefika wilayani Korogwe na kuzungumza na wanaCCM ikiwa ni wilaya yake ya kwanza kuitembelea tangu achaguliwe kuchukua nafasi hiyo Disemba 12, 2017 mjini Dodoma.

Aidha Dk. Mndolwa amevitaja vipaumbele vyake katika utendaji wake kuwa ni pamoja na kusimamia utawala bora ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) pia kulipa madeni yote ya watendaji ndani ya jumuiya ya wazazi katika kipindi cha siku mia moja za kwanza ndani ya Maharaja yake.

Jambo jingine lililozungumzwa na mwenyekiti huyo ni mikakati yake ya kurudisha nidhamu kwenye jamii ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Pombe Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles