31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

LEMA AWAONYA WATENDAJI TRA KUJIGEUZA POLISI

NA MWANDISHI WETU-ARUSHA


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amewaonya baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wanaotumia ukali na umakini wa Rais Dk. John Magufuli vibaya kama kigezo cha kuonea wafanyabiashara mjini hapa wakati wa ukusanyaji wa mapato.

Alisema mwenendo wa makusanyo mkoani hapa hayaridhishi kwani TRA wamegeuka kuwa jeshi, wanaonea na kudhalilisha watu pindi wanapokwenda kukusanya mapato.

Lema alisema kuwa ukali na umakini wa Rais Magufuli, umesaidia katika baadhi ya mambo, lakini pia umetumika kuongeza wigo mkubwa wa rushwa kwani kuna baadhi ya watendaji wanatumia nafasi hiyo  kujinufaisha, kuwaomba kwa  kuwalazimisha wafanyabiashara kuchangia masuala mbalimbali katika jamii.

“Mheshimiwa Rais tambua ukali wako na umakini kuna watu huku chini wanautumia vibaya, hawautumii kwa utendaji, ndiyo maana wanapenda vyombo vya habari sana, kwani kuna mambo ya giza mengi wanayofanya kuliko mambo ya nuru wanayofanya, watu wanateswa kuliko nyakati zozote katika taifa hili.

“Rais atambue kuwa ofisi za Serikali rushwa imekuwa ya kimfumo, rushwa ya kimabavu, wanatisha na kudhalilidha watu, TRA wanaenda kukusanya kodi kwa bunduki, Takukuru, Usalama wa Taifa wakati kodi ni maridhiano, wafanyabiashara wanatishwa,” alisema Lema.

Alisema kuwa hali hiyo ikiendelea itasababisha ukusanyaji wa mapato

nchini kushuka kwani wafanyabiashara hawatakuwa na ujasiri wa kuwekeza, mauzo yatapungua wakati  kodi inapatikana kupitia mauzo.

Lema alidai kuwa baadhi ya baa jijini hapa  zimekuwa zikivamiwa usiku na TRA wakiwa na polisi na kwenda kwenye droo za kaunta na kuangalia mauzo wakidai risiti na kwamba TRA wamegeuka kuwa waasi badala ya kukusanya kodi, hali inayosababisha usumbufu kwa wafanyabiashara.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles