Kwaya ya Healing Voice kuzindua ‘Kisa cha kale’

NA GLORY MLAY

KWAYA ya Healing Voice inatarajia kufanya uzinduzi wa albamu yao ya kwanza ya ‘Kisa cha kale’ Mei 29 mwaka huu.

Uzinduzi huo utafanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa na jumla ya nyimbo nane ukiwemo ‘Mpanzi’, ‘Sabto’, ‘Agano na mbingu zahubiri’ na nyingine nyingi.

Katika uzinduzi huo kwaya na vikundi mbalimbali vitatumbuiza vikiwemo Vocapella, The Flame, Soda ya Dhihu, Mbiu Choir Ushindi Youth Church, Light bearers, Born to Praise, Mashujaa wa Yesu, Jerusalem Singers, Acacia Singers.

Pia waimbaji binafsi kama Samweli Mhazini, Nuru Kitambo, Peter Machoke na wengine wengi wamealikwa kutumbuiza katika uzinduzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here