26.7 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Papa Wemba kuzikwa kesho

Mke wa marehemu Papa Wemba (wapili kutoka kushoto) Marie Rose, akifarijiwa na ndugu.KINSHASA, CONGO

MAZISHI ya nguli wa muziki nchini Congo, Papa Wemba, ambaye amepoteza maisha Aprili 24 nchini Ivory Coast, yamesogezwa mbele badala ya kuzikwa leo atazikwa kesho.

Inadaiwa kwamba rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila, aliiomba familia ya marehemu, Papa Wemba, kusogeza mbele mazishi hayo kwa ajili ya kuwapa nafasi wadau na marafiki wa marehemu wanaowasili leo nchini humo ili wawahi mazishi hayo.

Baada ya kifo hicho kutokea rais huyo alitoa ndege kwa ajili ya kuchukua maiti jijini Abidjan nchini Ivory Coast hadi Kinshasa.

Kifo cha msanii huyo hadi sasa kimekuwa na utata, huku kukiwa na habari kwamba aliwekewa sumu kwenye kipaza sauti chake na kumfanya apoteze maisha papo hapo baada ya kuanguka jukwaani, uchunguzi wa kifo chake unaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles