23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Muumini: Kupaza kanidhalilisha

muumini mwinjumaNA MWALI IBRAHIM

MKURUGENZI wa Bendi ya Double M Plus, Muumini Mwinjuma, amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya  mwanamuziki mwenzake wa bendi hiyo, Salehe Kupaza, aliyedai alimtwanga makonde.

Sakata hilo lilitokea Jumamosi mara baada ya bendi hiyo kumaliza kutoa burudani katika ukumbi wa Star Point, uliopo Kigogo ambapo Muumini alikataa kumpa posho mwimbaji wa kike, Amina kutokana na kutokufanyakazi siku hiyo.

“Amina amekuwa na tabia ya kuchagua nyimbo za kuimba na wakati mwingine hapandi kabisa jukwaani sasa juzi (Jumamosi) sikumpa posho kwa kuwa hakufanyakazi na Jumapili nilimuita kwenye kikao nijue kama anataka kuendelea na bendi au la, mara akaja Kupaza akaniambie nimpe Amina posho nikamtaka atuache kwa kuwa hajui makubaliano yetu.

“Wakati nilipotoka nje nikashangaa nimepigwa ngumi ya usoni na Kupaza, nikadondoka kama nilielekea kupoteza fahamu ndio watu wakanisaidia, nikaenda kuripoti kituo cha polisi cha Urafiki nikapewa PF3 nikatibiwa Palestina, bado nina maumivu kwenye jicho, Kupaza kanidhalilisha mbele ya mashabiki,” alisema.

Alisema kwa udhalilishaji huo hatokaa kimya, atahakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa huku akidai kwamba hataweza kufanyakazi naye tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles