27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mary Msigwa: Wasanii chipukizi hatuthaminiwi

MARY MSIGWANA GEORGE KAYALA

MWIMBAJI chipukizi katika muziki wa Injili nchini, Mary Msigwa, amelalamikia wasanii wenye majina makubwa katika muziki huo kutowathamini, vyombo vya habari na wadau wa muziki huo pindi wanapotaka msaada kwa ajili ya kukuza muziki wao.

Msigwa alilalama kwamba nyimbo za wasanii chipukizi hazipewi nafasi ya kuchezwa kwenye redio na runinga mbalimbali bila sababu za msingi.

Mary alisema changamoto nyingine zinazowakabili waimbaji wachanga ni kukosa fedha kwa ajili ya kurekodia, kushindwa kujitangaza kiasi kwamba wanashindwa kutambulika kwa jamii.

“Wasanii chipukizi hatuthaminiwi na hii imesababisha baadhi ya wenzetu kushindwa kuendelea na huduma hii kwani hata kama ukifanikiwa kurekodi kwa kujibana shida inakuwa kwa watangazaji wa redio na televisheni ambao huwa hawazipi nafasi nyimbo zetu na hii inasababisha tushindwe kufahamika kwenye jamii,” alisema mwimbaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles