24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mayanja: Tutashinda mechi zilizobaki

Mayanja-J-1NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

BAADA ya kujiondoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Jackson  Mayanja, amesema jukumu lake sasa ni kuhakikisha kikosi chake kinamaliza michezo yote iliyobaki bila kupoteza.

Timu hiyo tayari imejitoa kwenye mbio za ubingwa kufuatia sare ya bila kufungana na Azam FC, katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi watakamilisha ratiba ya ligi msimu huu kwa kuikabili Mwadui FC, Majimaji, Mtibwa Sugar na JKT Ruvu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema mipango yake ni kuiwezesha Simba kumaliza ligi ikiwa imeshinda michezo yote iliyosalia.

Mayanja alisema ni vema akautumia muda mfupi uliobaki, kuyafanyia marekebisho makosa mbalimbali yaliyojitokeza kwenye mechi za nyuma, ili waweze kufanya vizuri.

“Ninachokihitaji mimi ni ushindi au sare katika mechi zote zilizobaki na siyo kupoteza kabisa, naamini uwezo huo tunao.

“Kilichobaki ni kufanya vema kwenye mechi zetu, hakuna haja ya kuanza kufikiria ubingwa ambao tayari tumeshapoteza matumaini ya kuupata,” alisema Mayanja.

Mayanja alisema kinachotakiwa kufanywa na viongozi wa timu hiyo ni kuanza maandalizi ya msimu ujao mapema kwa kuangalia zaidi suala la usajili.

Simba imeendelea kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 58, huku ikizidiwa pointi saba na Yanga ambayo inaongoza kwa jumla ya pointi 65, wakati Azam FC wakiwa kwenye nafasi ya pili kwa pointi 59.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles