22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Azam alaumu wachezaji

dennis-KitambiNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA msaidizi wa Azam FC, Denis Kitambi, amewatupia lawama washambuliaji wake kwa kushindwa kufuata maelekezo ya walimu, kiasi cha kuyumbisha mwenendo wa timu hiyo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kitambi aliyasema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Simba na timu hizo kutoka sare ya 0-0, katika mechi ya ligi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kitambi alisema, sare hiyo imefifisha mbio zao katika kuwania taji la Ligi Kuu linaloshikiliwa na Yanga.

“Washambuliaji wetu wana kiwango kizuri, lakini hakuna faida ya kuonyesha uwezo bora ikiwa unashindwa kuipatia timu yao mabao.

“Tatizo hili limekuwa sugu sasa, tumejikuta tukitengeneza nafasi nyingi za kupata mabao na kushindwa kuzitumia na hili halijatokea kwenye mchezo huu tu, hata kwenye mechi za huko nyuma,” alisema Kitambi.

Kitambi alisema wamekuwa wakijitahidi kulifanyia marekebisho tatizo hilo wakitegemea kuona mabadiliko, lakini washambuliaji wao wameendelea kuboronga.

Timu hiyo ambayo inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi 59, leo inatarajia kuendelea na maandalizi ya mchezo wake ujao dhidi ya JKT Ruvu, ambao unatarajiwa kufanyika kesho katika Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles