23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kurasini wakataa nyumba zao kubomolewa bila utaratibu

Na CHRISTINA GAULUHANGADAR ES SALAAM

WANANCHI wa Mtaa wa Mivinjeni  Kata ya Kurasini, Dar es Salaam  wameiomba Serikali kuingilia kati utaratibu unaotaka kutumika kuwabomolea nyumba zao kwa kuwa umeghubikwa na sintofahamu.

Akizungumza Dar na Salaam mwishoni mwa wiki, Katibu wa wenye nyumba 50, Abbas Mkangala, alisema tangu waambiwe eneo lao anatakiwa mwekezaji hadi sasa hawajamfahamu na wanadhani kuna mchezo mchafu unataka kufanywa dhidi yao.

Alisema awali eneo hilo lilichukuliwa na mradi wa uendelezaji  upya Kurasini ukihusisha ujenzi wa Kituo cha Biashara cha Kimataifa (Tanzania China Logistic Centre)  ambao walikataa kipande cha hekta nane kwa madai kuwa halifai.

”Mwaka 1994 tulipewa hati eneo hilo liwe makazi maalum na mwaka 2017 tulipewa ramani ya viwanja na mipango miji,” alisema Mkangala.

Alisema wao hawakatai mradi kwa vile  unaweza kuleta maendeleo wanachopinga ni usiri uliopo sasa.

”Hatutaki tufanyiwe tathmini hapa katika eneo letu, tunachotaka tuletewe mwekezaji ndiyo tuongee naye tujue atalipaje,’ alisema Mkangala.

Alieleza kushangazwa na notisi wiki iliyopita zkiwajulisha kufanyika kwa tathmini katika eneo la mwekezaji  Seaglow Shipping Service ndani ya saa 48.

”Sisi kama wamiliki wa eneo hili tumeshangaa mno kwa sababu   huyo mwekezaji hatumjui na tunachofahamu mradi uliokuwepo tayari umepita … hivyo tunaamini kuna mchezo mchafu,”alisema Mkangala.

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo walikuwa wameshika mabango yenye ujumbe mbalimbali ambao ulikuwa ukieleza malalamiko yao juu ya mradi huo unavyotaka kuendeshwa.

Waandishi wa habari walimpigia simu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke, Subira Mwakabibi ambaye alisema hana taarifa ya tathmini hiyo mbali ya barua ya taarifa ya tathmini ya lazima kuonyesha imesainiwa na P.Masoy kwa niaba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles