27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jafo akerwa hospitali Wilaya ya Ilala kukwama

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Seleman Jafo, ameonyesha kukerwa kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika eneo la Kivule licha ya Serikali kutoa Sh bilioni 1.5 za ujenzi huo.

Wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, alilazimika kumnyang’anya kazi mkandarasi Kampuni ya Skoll Construction na kuukabidhi mradi huo kwa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT).

Akizungumza jana baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, Jafo alisema ameridhika na kasi ya ujenzi huo na kutaka manispaa nyingine za Dar es Salaam kuiga utendaji kazi wa Kigamboni.

“Nawapongeza kwa ujenzi wa hospitali naona mmeanza vizuri, niwaombe manispaa nyingine kwa Jiji la Dar es Salaam waje kujifunza utaratibu wa kufanya kazi Kigamboni.

“Wale wenzangu wa Kivule tangu nimesikia mpaka leo wanasema mchoro, ni jambo ambalo limenitia kichefuchefu sana toka 2016. Nashukuru kama DC ameamua kuingilia kati baada ya kuona kuna uzembe,” alisema Jafo.

Kuhusu jengo la ofisi za Manispaa ya Kigamboni, aliwataka Wakala wa Majengo Tanania  (TBA) kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo haraka ili ifikapo Juni 25 mwaka huu lianze kutumika.

“Nataka Juni 25 muhamie kwa sababu pale (zilipo ofisi za manispaa hivi sasa) mnatumia fedha nyingi kulipa pango,” alisema.

  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, alisema watajitahidi kusimamia miradi yote kwa ukamilifu na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora.

“Tumepewa zaidi ya Sh bilioni 20 kwenye miradi ya maendeleo ikiwamo afya, majengo ya watumishi na masoko ya kisasa. Tutaisimamia kwa ukamilifu na fedha za Serikali zitatumika ipasavyo,” alisema Sara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles