24 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kuna tatizo kwenye Sheria ya Habari-Wadau

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wadau wa Tasnia ya Habari nchini wamesema kuna tatizo kwenye Sheria ya Huduma za Habari nchini na kwamba ndiyo sababu yanahitajika mabadiliko.

Akizungumza Dar es Salaam juzi kwenye Semina ya kuwajengea uelewa wanahabari, Deodatus Balile ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema kuna tatizo kwenye sheria hiyo na kwamba, baadhi ya vipengele vinapaswa kuondolewa kabisa.

James Marenga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA – TAN).

“Sheria inaruhusu kesi yako kuendeshwa bila wewe mwenywe kujua. Kesi unaweza kufunguliwa Mwanza, siku unashuka mtaani unakutwa unapigwa tanganyikajeki.
‘’Ndio, wanaweza kiufanya hivyo, sheria inaruhusu. Tunapopigania hii sheria iondolewe ama ipitiwe upya, watu wajue tunapigania maslahi ya wengi,’’ amesema Balile.

Upande wake James Marenga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA – TAN) amesema, Sheria ya Uhalifu Mtandaoni ina maneno hatari yanayoweza kumuumiza mwandishi kwa kiwango kikubwa.

Akizungumza kwenye semina na wanahabari, leo jijini Dar es Salaam Marenga ambaye ni wakili wa kujitegemea amesema: “Tusipokuwa makini, sheria hizi zitaumiza wengi,” amesema Wakili Marenga.

Ametaja baadhi ya maneno yenye mitego katika sheria hiyo ikiwa ni pamoja na ‘kwa namna nyingine’ ama ‘kusudio na kinyume cha sheria.

“Neno kama ‘kwa namna nyingine ama kusudio na kinyume cha sheria,’ ni maneno hatari yanayotumika hasa kuharamisha jambo ambalo sio kosa kisheria. Maneno haya unaweza kuyaona kuwa ya kawaida, lakini ni hatari sana,” amesema Wakili Marenga.

Kwenye semina na wanahabari hao, Wakili Marenga amesema, kwenye sheria hiyo kuna adhabu zilizowekwa kwa makosa ambayo hayapo wazi kinyume na Ibara ya 13 (6)(C) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia amesema, sheria hiyo kupitia Kifungu 7 (i)(g) iliyotungwa mwaka 2015, imevuruga uhuru wa faragha ambapo taarifa binafsi za mtu zinaweza kuchukuliwa na polisi kinyume na Ibara ya 16(i) ya Katiba ya Tanzania.

“Sheria hii katika Kifungu cha 50(2)(b) kinaondoa haki ya mtu kukata rufaa kinyume na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, lakini pia Kifungu cha 38(2)(b) cha sheria hii kinaruhusu usikilizwaji wa shauri mahakamani hata bila muhusika kuwepo.

“Hukumu ikitolewa, ndio unatafutwa na kufungwa bila kujua kesi yako ilipelekwa mahakani lini, na kwa kosa gani. Ndio maana tunasehma sheria hii inatakiwa kupitiwa upya,” amesema Wakili Marenga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles