27.4 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali kutumia Bilioni 700 kuhamisha kaya 22,000 Hifadhi ya Ngorongoro

Ramadhan Hassan, Dodoma

SERIKALI imesema wastani wa Sh bilioni 700 zitahitajika kwa ajili ya kuhamisha kaya 22,000 zilizoko eneo la Hifadhi la Ngorongoro ikiwa wananchi wote watataka kuondoka ili kupisha Ikolojia ya uhifadhi kwenye eneo hilo.

Hayo yameelezwa leo jijini hapa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Dk. Christopher Timbuka wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Dk. Timbuka amesema kiasi ni kikubwa lakini kwa namna ya umuhimu wa eneo hilo, fedha hizo ni ndogo na zinaweza kupatikana kwa muda mfupi kutoka kwenye eneo husika hasa kama shughuli za binadamu zitapungua.

Amesema hadi Julai 18,2022 kaya 757 zenye idadi ya watu 4,344 na mifugo 8,276 zilishajiandikisha kuhama kutoka Ngorongoro kwenda kijiji cha Msomela Wilaya ya Handeni ambako zoezi linaendelea hadi sasa.

Amesema idadi ya watu wanaohama katika eneo hilo wanaendelea kujiorodhesha kwa kasi ambayo hawakuitegemea hivyo kuna kila haja ya kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba na miundombinu ya kuwapokea katika eneo hilo ambayo ni rafiki kwa shughuli za ufugaji na kilimo.

“Ni kweli gharama za kuhamisha watu ni kubwa, lakini mapato yanayotokana na eneo hilo na hasa yakishakuwa wazi yataongezeka zaidi kwa hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwenye zoezi hili,” amesema Dk. Timbuka.

Mhifadhi huyo amesema serikali inafanya mkakati wa kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na utalii hadi kufikia watalii milioni 1.2 na mapato kufikia Sh bilioni 260 ifikapo mwaka 2025.

Kutokana na hali hiyo wamewaomba wakazi wa maeneo hayo kuendelea kujiorodhesha ili waweze kuhama kwani hata huko wanakwenda kuna manufaa makubwa kuliko wanakotoka.

Amesema baadhi ya faida za kwenda Msomela ni kumilikishwa ardhi, kuwa na nyumba za kudumu,pamoja na mashamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles