23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

S3 Education yahimiza wazazi kuitumia ili watoto wapate elimu bora nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Elimu ya S3 Education Limited imewasihi wazazi na wanafunzi kuitumia ili kuwawezesha kupata vyuo bora nje ya nchi.

Akizungumza na Mtanzania Digital katika maonyesho ya Vyuo vya Elimu ya Juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam, Mwakilishi wa taasisi hiyo, Fatema Salemwalla amesema lengo lao ni kuwasaidia wanafunzi wa kitanzania kupata vyuo kwa urahisi.

“S3 Education Limited ni taasisi iliyosajiliwa na (UCAS) ambayo inajihusisha na kuwatafutia vyuo vya nje ya nchi wanafunzi wanaotaka kusoma katika nchi za Uingereza, Dubai, Canada, Marekani, Australia , Malaysia , China, India, Afrika Kusini, Mauritius na nyingine nyingi,” amesema Fatema.

Aidha, amefafanua kuwa mbali na kuwanunganisha wanafunzi na vyuo hivyo pia wamekuwa wakiwasaidia katika kufanya udahili, ushauri na huduma ya kusafiri.

“Tunawasaidia kutafuta Visa, ushauri juu ya chuo gani bora mwanafunzi anatakiwa kwenda kulingana na ufaulu wakewa masomo.

“Pia tunatoa huduma kwa mwanafunzi kabla ya safari bure bila malipo, hivyo mzazi au mwanafunzi anaweza kutembelea kwenye ofisi zetu zilizopo Upanga jirani na Shule ya Shaaban Robert kwenye jengo la Girl Guides, hivyo milango iko wazi muda wote au mtu anaweza kutembelea tovuti yetu ya www.s3education.com ,” amesema Fatema.

Katika hatua nyingine amewataka Watanzania kutembelea kwenye banda lao lililoko katika maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles