29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU AGOSTI 2017 UHURU KENYATTA: KWANINI NASTAHILI MUHULA WA PILI

APRILI 9, mwaka huu Rais Uhuru Kenyatta alitimiza miaka minne tangu aapishwe kuiongoza Kenya.

Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha kipindi hicho cha miaka minne ya utawala wake alitoa hotuba akieleza kwanini anastahili kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili kutokana na kile alichotaja kuwa ufanisi mkubwa chini ya utawala wake.

Kama ilivyotafsiriwa na mwandishi wetu tunawaletea hotuba yake hiyo;

Aprili 9 ni siku maalumu na kukumbukwa mno kwangu, na kwa mamilioni ya Wakenya. Miaka minne iliyopita, katika siku kama hii, nilichukua kiapo cha uaminifu na utii wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kirais.

Nilifanya viapo hivyo nikijua uzito wa majukumu niliyobeba, na uaminifu mkubwa nilioaminiwa na raia wa Kenya.

Imekuwa miaka minne sasa na kila siku ipitayo, maneno ya kiapo yamekuwa ilani katika maamuzi na matendo yangu. Namshukuru Mungu kwa fursa hii tukufu niliyopewa kuwatumikia watu wangu na kuwa sehemu ya mafanikio ya ukuaji huu wa Kenya.

Ninajivunia kuwa ugatuzi umetekelezwa kikamilifu. Naamini historia hii itakumbuka jukumu ambalo utawala wangu ilikuwa nalo katika kuleta mabadiliko katika nchi yetu.

Kuhakikisha kwamba kaunti zinaanzishwa na kufanya kazi kama inavyopaswa katika utawala wangu kwa mujibu wa ratiba. Juhudi zetu zilifanywa katika utimilizo wa kiapo changu cha utii, kuiheshimu, kulinda na kuitetea Katiba, na pia kwa sababu ninaamini ugatuzi ni mfumo mzuri wa utawala wa serikali.

Kulinda uhuru na heshima ya taifa letu, nimefanya kazi kwa bidii kuleta mabadiliko chanya katika vikosi vyetu vya usalama kuweza kulinda watu na kila inchi ya Kenya.

Tumeweza kuongeza idadi ya askari polisi, kuboresha maslahi yao kwa kujua kwamba molari nzuri ni muhimu katika kujenga jeshi imara.

Tumewekeza katika teknolojia na vifaa, kuimarisha uratibu wa usalama na kuufanya kuwa kipaumbele namba moja.

Wakati linapokuja suala la ugaidi, tumeongeza uwezo wa kubaini na kupangua njama za kigaidi, kuhakikisha uwapo wa uratibu na ushirikishaji ndani ya serikali na miongoni mwa raia.

Kwa sababu ya hatua hizo, idadi ya mashambulizi imeanguka kwa kiasi kikubwa. Lakini bado kuna sehemu za Kenya, ambazo hazina usalama na, ambazo ghasia za kihalifu zinaendelea kukwamisha ustawi wa kimwili na kiuchumi wa watu wetu. Hatujalala katika kuchukua kurudisha usalama katika maeneo hayo yaliyoathirika.

Chaguzi zijazo zitakuwa muhimu mno kuonesha uhuru wa kujiamulia mambo wa watu wa Kenya. Viapo vyangu kama Rais ni kufanya kila linalowezekana ili chaguzi hizi ziwe za amani.

Wakenya kwa bahati mbaya wamekuwa mashuhuda wa siasa za vurugu, ambapo siasa za kutokubaliana zinachukuliwa na makabiliano ya vurugu.

Hili halitaruhusiwa kuota mizizi. Nimechukua na nitaendelea kuchukua, kila hatua kuhakikisha vikosi vya usalama vinaandaliwa kuzuia na kukabili machafuko hayo ya kisiasa.

Hakuna yeyote nchini Kenya anayestahili kucheza nje ya sheria na Katiba yetu, si kiongozi wala raia wanaopaswa kuhujumu mfumo na kuleta mgawanyiko au mgogoro.

Natoa mwito kwa Wakenya kukataa aina hiyo ya uongozi. Kwa upande wangu, nitatimiza kiapo changu na kufanya haki na kwa ajili ya usalama wa Wakenya bila hofu, upendeleo,  au nia mbaya.

Niliapa kulinda heshima ya Kenya na Wakenya wote. Katikati ya heshima hiyo ni kwamba Wakenya wanapaswa kutendewa kwa haki na ubinadamu, na kwamba wanapaswa kuwa na uhuru wa vitendo kisheria.

Katika Kanisa la Katoliki nilimokulia ni kwamba heshima inakuja na uumbaji wa mwanadamu katika taswira na mfano wa Mungu na hautengani na uhuru wa mtu.

Nimeweza kulinda heshima hiyo kipindi cha miaka minne iliyopita. Kwa nchi, hakuna shaka hadhi na heshima yetu mbele ya kusanyiko la mataifa imepanda. Leo hii, Kenya ni mshirika muhimu wa amani na usalama wa kikanda na utoaji maamuzi duniani.

Ni heshima ya kuona heshima kubwa waliyo nayo watu wetu. Hata kama ni hali ngumu, Wakenya wanajivunia na kuwa na matumaini ya wakati ujao.

Nimeshuhudia Wakenya wakisisitiza njia ngumu kuelekea utimilizo wa ndoto zao ziendelezwe na viongozi wao. Huo ni wajibu muhimu wa uongozi na nalichukulia kwa uzito mkubwa. Hivyo, pia niamini umasikini unanyima heshima ya Wakenya wengi.

Ndiyo maana nimefanyia kazi matarajio na kuweka msingi wa uchumi ulio tayari kuendelezwa kiviwanda na kutengeneza mamilioni ya ajira kutoka sekta ya uzalishaji zinazohitajika kwa Wakenya.

Haitoshi kucheza na uchumi, unahitaji mageuzi iwapo unataka kufikia ndoto za watu wetu.

Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya kiwango cha standard ni mfano hai wa ndoto zetu. Uwekezaji mkubwa tangu uhuru wetu umekuja kwa mujibu wa bajeti na ratiba.

Ni teknolojia mpya, zilizoandaliwa kuleta mageuzi ya kilimo na biashara, na bila kusahau hitaji la urithi mzuri wa wanyamapori. Wakenya watasafiri katika treni kipindi cha wiki chache zijazo na tutaona mwanga wa wakati ujao ambao u tayari ukionekana.

Ajira zaidi na nzuri zitakuwa matokeo ya juhudi zangu za kubadili gia za uchumo wetu. Ajira hizo na kuimarika kwa ustawi, pamoja na mageuzi ya uchumi wetu uliobakia kutoka kukua kwa sekta ya uzalishaji, ongezeko la thamani na biashara itainua heshima ya mamilioni ya watu wetu.

Kuna mengi ya kufanya, kuleta mageuzi katika nchi, chumi na mifumo ya serikali huchukua muda.

Tumefanya mengi kipindi cha miaka minne kuliko nchi nyingi zilivyoweza kufanya kwa miongo kadhaa. Tumeweka msingi, tumeonesha kwamba Kenya inaweza kuendana na ratiba na bajeti.

Dunia imeshuhudia na ninataka kila Mkenya kufahamu ya kwamba tuko njiani kuelekea katika nchi ya ahadi yenye fursa na usalama.

Ninawania urais kwa mara nyingine ili nikamilishe kazi ya kulijenga taifa hili kubwa ling’are  kwa viwango vya Afrika na Dunia. Hivyo, Mungu anisaidie.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles