25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

KOREA KASKAZINI: TUTAFANYA MAJARIBIO YA MAKOMBORA KILA WIKI

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI


MAMLAKA za Korea Kaskazini zimesema zitaendelea kufanya majaribio ya makombora yake licha ya kelele za jumuiya ya kimataifa.

Akizungumza na mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), John Sudworth, Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Han Song-ryol alisema watatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila wiki, kila mwezi na kila mwaka.

Awali, Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence, aliionya Korea Kaskazini kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.

Pence aliwasili Korea Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kombora la Korea Kaskazini kushindwa kuruka.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika Peninsula ya Korea wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea Kaskazini na Marekani.

Han alionya; “Iwapo Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi yetu, tutachukua hatua ya kupambana kwa shambulio la nyuklia kwa mbinu zetu na mtindo wetu,” alionya Han.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,207FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles