25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

KUACHANA KWAMRUDISHA JANET JACKSON KWENYE MUZIKI

LONDON, ENGLAND


MSANII wa muziki wa pop nchini Marekani, Janet Jackson (50), ameweka wazi kwamba kwa sasa yupo huru kufanya mambo yake na anajiandaa kurudi kwenye kazi yake ya muziki baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Wissam Al Mana, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Msanii huyo ameonekana juzi kwa mara ya kwanza akiwa na mtoto wake ambaye hajawahi kuonekana tangu alipozaliwa miezi mitatu iliyopita.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Janeth aliandika kwamba, baada ya kuachana na mume wake huyo yupo huru kufanya mambo yake ikiwamo muziki ambao anadai wakati akiishi na mwanamume huyo hakutaka afanye muziki.

“Muda mfupi ujao nitaanza kuendelea na harakati zangu kama awali, nilikuwa kwenye ndoa nikawa nashindwa kufanya baadhi ya mambo, lakini kwa sasa nipo huru nikimlea mwanangu na muda mfupi nitarudi kwenye kazi yangu ya muziki iliyonipatia fedha na jina kubwa,’’ alisema Janet.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,717FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles